Askari polisi waliosuka nywele za mitindo waagizwa kuzifumua kabla ya januari 1,2020

Naibu
Inspekta Jenerali wa Polisi Edward Mbugua, ameonyesha wasiwasi juu ya
maafisa wa polisi waliOsukwa nywele zenye mapambo ya kuvutia jambo
ambalo ni ukiukaji wa sheria.

Maafisa wote wa kike watalazimika kufumua nywele walizosukwa
zisizoendana na sheria ya mavazi ya polisi kuanzia tarehe 1, 2020, kwa
mujibu wa idara ya Polisi nchini Kenya.
“Kuna haja ya kutambua kwamba sare ya polisi ni ishara ya mamlaka na
inastahili kupewa heshima yake. Kuanzia Januari 1, 2020, nywele za
mitindo isiyokubalika hazitakubaliwa,” Bwana Mbugua amethibitisha.
Maafisa wa kike wa polisi nchini Kenya watatakiwa kuondoa mitindo yao ya
nywele pamoja na zile walizobandika katika kipindi hiki cha sikukuu.
Idara hiyo ya polisi inasema inataka kuhakikisha maafisa wote wanafuatilia kikamilifu mfumo wa mavazi rasmi ya kazi.
Aidha hatua hii inaenda sambamba na sare mpya za polisi zilizotolewa.
Taarifa iliyotolewa mapema wiki hii, inasema kwamba makamanda wote wa
polisi wa eneo wamepewa jukumu la kuhakikisha kwamba sheria ya mavazi
inafuatiliwa vilivyo.Inspekta Jenerali Mbugua amedai kuwa mitindo ya
nywele zilizosukwa inafanya iwe vigumu kwa maafisa hao kuvaa kofia zao
wakiwa kazini.
Taarifa hiyo iliyotiwa saini na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Edward
Mbugua, ilionyesha wasiwasi kuhusu maafisa wa polisi walisukwa nywele
zao zilizowekwa mapambo ya kuvutia na kukiuka mavazi rasmi ya polisi.
Katika taarifa hiyo iliyotolewa Desemba 20, 2019, Bwana Mbugua anasema
kwamba upambaji wa nywele kwa nakshi kupita kiasi ni ukiukaji wa kanuni
za idara ya Polisi.
“Katika ziara yangu rasmi ya kikazi sehemu mbalimbali nchini katika
kipindi cha wiki moja iliyopita, nimeshuhudia maafisa wa ngazi
mbalimbali hususan wa kike wakiwa wamesuka nywele zao kwa namna
isiyokubalika,” Mr Mbugua amesema.
Kuanzia tarehe Mosi Januari, 2020, polisi wanawake nchini Kenya
watatakiwa kufuata kikamilifu sheria na kanuni za mavazi ya polisi
nchini huo.
Sare ya Polisi
Inspekta Jenerali Mbugua amedai kuwa mitindo ya nywele zilizosukwa
inafanya iwe vigumu kwa maafisa hao kuvaa kofia zao wakiwa kazini.
Bwana Mbugua ameonyesha wasiwasi wake juu ya hijabu za rangi kwa
Waislamu akikisitiza kwamba wanastahili kuvaa hijabu rasmi nyeusi ya
kitambaa chembamba kulingana na sheria.
“Nimeshuhudia vazi la kuhifadhi kichwa kwa Waislamu lililobadilishwa
kulinganisha na makubaliano ya awali yaani kutoka mtandio mweusi hadi
ile yenye rangi,” amesema.
Chanzo – BBC