Karani wa ikwabansabo amcos kwa tuhuma za kutoroka na milioni 15 za wakulima wa pamba

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanri akiwahutubia viongozi na wafanyakazi wa Wilaya ya Nzega hivi
karibuni wakati wa mkutano wa majumuisho ya ziara yake ya siku tatu ya
kuhamasisha kilimo ikiwemo pamba na upandaji wa miti. 
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanri akiwahutubia viongozi na wafanyakazi wa Wilaya ya Uyui  hivi
karibuni wakati wa mkutano wa majumuisho ya ziara yake ya siku nne ya
kuhamasisha kilimo ikiwemo pamba na upandaji wa miti.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya
akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa
ajili ya kuwahutubia viongozi na wafanyakazi wa Wilaya ya Uyui  hivi
karibuni wakati wa mkutano wa majumuisho ya ziara yake ya siku nne ya
kuhamasisha kilimo ikiwemo pamba na upandaji wa miti. 
********************************************

MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameliagiza Jeshi la
Polisi wilayani Nzega kumsaka na kumkata Karani wa Chama cha Msingi cha
Ushirika cha Ikwabansabo kwa tuhuma za kutoroka na shilingi milioni 15.9
za wakulima wa pamba.

Alisema mtuhumiwa huyo ambaye ni Raphael Malimbi alikiuka
taratibu za uchukuaji wa fedha kwa ajili ya malipo ya mauzo ya pamba ya
wakulima ambapo alichukua fedha taslimu badala ya kuwalipa kupitia
akaunti za wakulima za Benki au simu za mkononi.

Mwanri alitoa kauli hiyo jana wakati wa mkutano wa majumuisho
na watendaji wa vijiji , kata , Maafisa ugani na Watumishi wa Wilaya ya
Nzega ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake ya siku tatu kuhamasisha
kilimo cha mazao mbalimbali ikiwemo pamba.

Alimtaka Kamanda wa Polisi Wilaya(OCD) ya Nzega SSP
Constatine Mbogambi kuhakikisha ndani ya saa 24 mtuhumiwa anamkamatwa na
kuanza taratibu za kumchululia hatua za kisheria ikiwemo kumfikisha
Mahakamani.

Mwanri alisema hatua ya kwanza ya kufanikisha hilo ni vema
Jeshi la Polisi likaanza kwanza kumkata Diwani wa Kata ya Milambo Itobo
ambaye ndiye aliyedhamini mtuhumiwa na kudai kuwa atalipa pesa hiyo ya
wakulima.

Alisema Serikali haiwezi kukubali vitendo vya kuwadhulumu
wakulima fedha zao vikaanza upya kwani ndivyo vilivyosababisha
wakachukia ushirika katika miaka ya nyuma.

Mwanri aliwaonya viongozi wengine ambayo wamechaguliwa
kusimamia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kutodiriki kugeuza
Ushirika ni sehemu ya kujipatia fedha kinyume cha sheria.

Alisema kama kuna kiongozi amejiingiza katika uongozi wa
AMCOS ili kupata utajiri amekosea njia ni vema akaondoka mapema kabla ya
hatua mbalimbali dhidi yake hazichukuliwa.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa aliwaonya Maafisa
Ushirika wa Halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha wanajiridhisha
uhalali wa malipo kabla ya kuyapitisha.

Alisema ikibainika kuwa Afisa Ushirika yoyote alishiriki katika malipo machafu atachukuliwa hatua ikiwemo kufukuzwa kazi.

Aidha Mwanri alisema kama kuna wakulima wa Pamba ambao bado
wanadai ni vema Maafisa Ushirika hao wakaorodhesha majina ya wakulima
ambao bado wanadai na kuyapeleka kwa Wakuu wa Wilaya kwa ajili ya
kufuatilia malipo ya wakulima.