Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi akimjulia hali mmoja wa
wagonjwa waliolazwa Hospitali ya Rufaa Dodoma kwa kile kinachodaiwa kula
chakula chenye sumu.

Mkuu wa Wilaya Dodoma (kushoto) Mhe Patrobas Katambi akiwa na Mstahiki
Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Devis Mwamfupe baada ya kufika
hospitalini hapo kujionea hali za wagonjwa 37 waliofikishwa na kulazwa
baada ya kudaiwa kula chakula chenye sumu.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi (mwenye koti la suti)
akiwa na wauguzi na madaktari wa Hospitali ya Rufaa Dodoma alipofika
kuwajulia hali wagonjwa waliofikishwa hospitalini hapo ambao wamepata
mgonjwa wa kuhara na kutapika wakihisiwa kula chakula chenye sumu

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Best Magoma akizungumza na wandishi
habari juu ya tukio la kulazwa kwa watu 37 katika Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Dodoma kwa kile kinachoelezwa kula chakula chenye sumu.

Watu mbalimbali walioleta wagonjwa wao katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
wa Dodoma wakisubiri kupata huduma kwenye kitengo cha dharura.

***
Charles James, Michuzi TV
Watu 37 wamefikishwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Dodoma (General Hospital) kwa ugonjwa wa kuhara na kutapika baada ya
kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu.

Tukio hilo limetokea jioni ya leo katika eneo la Mtumba nje kidogo ya
Manispaa ya Jiji la Dodoma ambapo walikula chakula hicho wakiwa kwenye
msiba wa jirani yao.

Akizungumza hospitalini hapo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama
ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi amekiri
kutokea kwa tukio hilo na kueleza tayari ameshaagiza vyombo vya ulinzi
na usalama kufanya uchunguzi kwenye mabaki ya chakula hicho ili kugundua
chanzo chake.

“Mara baada ya kupata taarifa hizi tumefika hapa na Timu ya viongozi wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama wa kwa hatua ya awali tumesimamia
kuhakikisha watu wetu wanapata huduma ya kwanza na kiukweli wagonjwa
wote wanaendelea vizuri.

Kati ya hao 37 waliolazwa, wanaume ni 10, wanawake wapo 23 na watoto
wakiwa ni wanne, tayari nishatoa maagizo kwa Jeshi la Polisi kufanya
uchunguzi wa kina kujua chanzo, lakini pia tunafanya uchunguzi wa
kitabibu kujua ni sumu ya mtu kuweka au ni sumu ya chakula,” Amesema Mhe
Katambi.

Amewataka wananchi kuwa watulivu kwa sasa na kusubiria kupata majibu
kutoka kwa Timu inayofanya uchunguzi na kuwataka wale wote ambao wanaona
dalili za kuhara na kutapika kufika katika vituo vya afya vilivyopo
karibu ili kupatiwa matibabu.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Best Magoma amesema hali
ya wagonjwa waliofikishwa hospitalini hapo inazidi kuimarika baada ya
kuwapatia matibabu na pindi watakaporidhishwa na maendeleo ya afya zao
wataruhusiwa kurudi majumbani mwao.

” Tunawashukuru viongozi wetu wa ngazi ya Wilaya wakiongozwa na Mkuu wa
Wilaya kwa kufika hapa na kutuongezea nguvu, na timu yetu kwa
kushirikiana na wenzetu wa Polisi na TBS tumeshaanza uchunguzi wa
kubaini nini chanzo cha tatizo hili, nitoe wito kwa wananchi ambao
wanaona dalili kama hizi kujitokeza haraka kwenye vituo vya afya na sisi
tupo tayari kuwahudumia,” Amesema Dk Magoma.