Tume ya vyuo vikuu -tcu yavifutia usajili vyuo 9 tanzania

Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) imefuta hati za
usajili wa vyuo vikuu vishiriki vitano, vyuo vikuu vitatu na chuo kikuu
kishiriki kimoja.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Januari 21, 2020 jijini
Dar es Salaam katibu mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa amesema
vyuo hivyo vimeshindwa kujirekebisha na hata vingepewa muda zaidi
visingeweza.
Amesema vyuo vishiriki ni Chuo kikuu kishiriki cha Askofu Mkuu Yakobo
(AJUCO), Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Kardinali Rugambwa (CARUMUCo) na
Chuo kikuu cha Theofilo Kisanji (Teku- Dar es Salaam), Chuo kikuu cha
Mtakatifu Yohana cha Tanzania kituo cha St Marks na Chuo kikuu cha Jomo
Kenyatta cha Kilimo tawi la Arusha (JKUA).
TCU pia imefuta hati za usajili wa vyuo vitatu ambavyo ni Chuo kikuu cha
Josiah Kibira (Kagera), Mount Meru (Arusha), IMTU (Dar es Salaam). Chuo
kikuu kishiriki kilichofutiwa usajili ni Chuo Kikuu cha Bagamoyo
(Pwani).