Tanesco ipo tayari kuunga mkono juhudi za serikali


NA FARIDA SAIDY,MOROGORO 

Shirika la umeme Tanzania TANESCO
limesema lipo tayari  kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya
awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Mafuli,ya kuleta
maendeleo kwa wananchi, ambapo kwa mala ya kwanza shirika hilo limetoa
gawio kwa serikali la shilingi bilioni 1.436.

Akizungumza wakati akifunga
mkutano wa baraza kuu la 49 la wafanyakazi wa tanesco mkoani Morogoro
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanesco Dkt Alexander Kyaruzi
alisema kuwa huo ni mwanzo mnzuri kwa shirika  katika kuleta maendeleo
ya taifa,ambapo serikali inamiliki hisa za shirika hilo asilimia mia
moja.

Katika hatua nyingine aliwataka
wasimamizi wanaosimamia miradi  ya kusafirisha umeme wa msongo wa
kilovati 400 wa Singida –Arusha hadi Namanga ,na ule wa iringa –mbeya 
hadi Tunduma kuharakisha miladi hiyo ili kufanikisha adhima ya serikali
ya awamu ya tano ya kuunganisha mifumo miwili ya gridi ya taifa ya nchi
za kusini mwa afrika(SOUTHERN AFRICA POWER POOL-SAPP)  na ule wa nchi za
afrika mashariki (EASTERN AFRICA POWER POOL-EAPP)inafanikiwa.

 Aidha aliongeza kuwa kukamilika
kwa miladi hiyo ya kusafirisha umeme wa kilovati 400 na ule wa kuzalisha
umeme wa Julius nyerere (JULIUS NYERERE HYDROPOWER PROJECT
–JNHPP)utaifanya Tanzania kuwa kati ya nchi zinazouza  umeme kwa mataifa
mengine .

Sambamba na hayo  Dkt Kyaruzi
amewataka wafanyakazi wa Tanesco kuwa makini pindi wawapo katika
majukumu yao ya kazi,hususani wanapokuwa safarini kwa kuhakikisha
madereva wa shirika hilo wanafuata sheria za usalama barabarani,haswa
katika swala zima la spidi wawapo safarini