Maafisa tcra waendelea kuchanja mbuga kampeni ya mnada kwa mnada hadi mikoa ya nyanda za juu kusini, wakazi njombe wafurika kujisajili

Foleni ya Wananchi wa Mji Mdogo wa Makambako na viungo vyake wakiwa katika mistari ya kupata namba za vitambulisho vya Taifa
Mkuu wa Nyanda za Juu Kusini wa TCRA Asajile John akizungumza na
Wananchi wa Makambako wakati wa usajili wa laini za simu kwa alama.
Add caption
Afisa
Habari Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel
Masasi akizungumza na Wananchi wa Mji Mdogo wa Makambako wakati wa
Kampeni ya Mnada kwa Mnada wa Uhamasishaji wa Wananchi kujisajili laini
za simu kwa alama za vidole.
::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
Wakazi wa Makambako mkoani Njombe na viunga vyake
 wamejitokeza katika kupata namba za vitambulisho vya Taifa ili kukidhi
matakwa ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania TCRA ipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya
 Uhamasishaji wa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.


Kampeni
 ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu
Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya
Uhamiaji  kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa
kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa
kuweka alama za vidole kwa laini za simu.
Kampeni
tangu imeanzishwa imekwenda katika maeneo ya miji na Mkoa lengo Wananchi
kutumia fursa ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole ambayo
unakwenda nchi nzima

 Mkuu
wa Nyanda za Juu Kusini  wa TCRA  Asajile John   amesema ni fursa kwa
wananchi wa Mkoa wa Njombe katika Mji Mdogo wa Makambako kufika katika
Viwanja vya idara ya maji kupata namba ya kitambulisho cha Taifa katika
mfumo wa NIDA.

 Amesema
katika Kampeni hiyo imekuwa inafanywa na kanda hiyo ili kila mwananchi
aweze kuwa na namba ya vya Taifa au kuwa na kitambulisho kutokana
Ushirikiano na NIDA kuwa katika Kampeni hiyo.

John
 amesema kuwa  Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya
Wananchi kuhudumiwa kwa pamoja huduma za mawasiliano pamoja na usajili
wa laini za simu kwa alama za vidole.

Amesema
Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika  huduma  za simu pamoja
kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi na kuongeza kuwa muda
ulioabakia ni mdogo hivyo kila mtu atumie kutafuta taarifa zinazokidhi
usajili wa laini kwa alama za vidole.

Hata
hivyo amesema  kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa
elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto
wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Hata hivyo amesema kuwa  kuna
watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi
Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kutoa elimu kuhusiana
 makosa ya jinai ya matumizi ya simu yasiofuata sheria.

Amesema
Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila
mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia
kitambulisho cha taifa.

Amesema  TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili watumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

Hata
hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za
vidole kabla ya Desemba 31 na muda uliobakia ni mdogo tangu tangazo
lilipotolewa.

“TCRA
tutahakikisha tunawafikia katika wananchi katika utoaji wa elimu za
utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma
hiyo” amesema.John

Ameongeza kuwa  Kampeni hiyo imeanza kwa Mikoa yote iliyopo katika Nyanda za Juu Kusini.

Nae
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa wananchi
wameitikia kwa kujitokeza kwa wingi  kuangalia namba  vitambulisho kwa
ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole.
Masasi
amesema kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA
kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika
mamlaka husika kupata vitambulisho.