Sadc kuwa na visa moja kupunguza urasimu



Ahmed Mahmoud/Arusha



Naibu Katibu
Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Thembinkosi Mhilongo amesema umoja huo umedhamiria kuwa na VISA moja kwa lengo la kupunguza urasimu ndani ya Jumuiya
hiyo

Image result for Dkt Thembinkosi Mhlongo
Hayo
yameelezwa leo na Naibu Katibu Mtendaji Mkuu wa SADC Dkt Thembinkosi Mhilongo wakati
wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wenye dhamana na Wizara za Mazingira,Maliasili  na Utalii katika nchi hizo za Ukanda wa
Kusini mwa bara la Afrika (SADC).


Dkt Mhilongo
pia amesema nchi za SADC zimejipanga 
kuangalia kwa kina   suala la
Viumbe na Mimea vamizi katika nchi  hizi
wanachama  pamoja na Wanyama ambao wako katika hatari ya kutoweka
katika nchi hizo.


Naibu Mtendaji
Mkuu huyo wa SADC amewataka Mawaziri  hao
wenye dhamana ya mazingira, maliasili na utalii kuhakikisha  wanaangalia kwa kina Itifaki na Mikataba  inayohusu Sekta hizo tatu katika nchi
Wanachama za SADC 



Amesema Mkutano
wa Mawaziri hao ni muhimu katika kukuza na kuchangia katika ukuaji wa uchumi
wa mataifa ya SADC h
ivyo
amewataka wakati wa Mkutano huo kupima na kuangalia kwa kina
  Sera na Itifaki zinazosimamia  Sekta hizo tatu ambazo ndio muhimili mkuu wa
Uchumi wa mataifa hayo.


Mbali na kuangalia
masuala hayo Naibu Mtendaji Mkuu huyo wa SADC amewataka Mawaziri hao
kuhakikisha wanaangalia  kwa Kina Sheria zote zinazosimamia  na kuongoza Sekta
hizo katika Jumuiya.




Amesisitiza
kuangaliwa upya Itifaki ya Utalii, Mazingira, na Maasili katika nchi Wanachama
za SADC na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na 
umuhimu kwa Mawaziri hao kuhakikisha majandiliano ya Mkutano wao yanalenga katika
kutatua changamoto zinazokabili sekta ya mazingira, maliasili na Utalii katika
nchi za SADC


Nchi za SADC
imebahatika kuwa na raslimali  lukuki
zikiwemo za Wanyamapori, misitu, Uvuvi 
rasilimali ambazo  ni muhimu katika
kuchangia ukuaji wa Uchumi na maendeleo ya  nchi wanachama za SADC.


Amewataka
Mawaziri hao kuangalia kwa kinja Itifaki 
ya SADC  inayohusu umuhimu wa
kusimamia na kulinda uhifadhi, kuangalia Itifaki ya misitu, Uvuvi na  Sheria ya usimamizi wa Wanyamapori


Pia
amesisitiza umuhimu kwa SADC Kutambua umuhimu wa kusimamia , kulinda na
kuhifadhi misitu ili kuwa na uhifadhi endelevu katika nchi hizi za Ukanda wa
Kusini mwa Afrika


Naibu
Mtendaji Mkuu huyo amesema Jiji na Mkoa wa Arusha limebeba  historia 
kubwa ya SADC kutokana na kuwa Jiji hili ndipo chimbo kubwa la
kuanzishwa kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika miaka 40 iliyopita


Amesema SADC
iliasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mzee Keneth Kaunda wa Zambia,
Rais Somora Machel wa Msumbiji, Rais Agustino Neto wa Angola na Rais Gabriel
Mugabe wa Zimbabwe ambapo Jumuiya hiyo iliasisiwa katika Ukumbi huo wa AICC


Aidha Mkataba
wake ulisainiwa Lusaka Nchini Zambia  kwa
ajili ya kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ambapo Makao ya SADC yapo Gaboro Nchini Botswana


Kukosekana kwa Visa moja  kwa Watalii  ulaya wanapokuja  katika ukanda huu wa kusini mwa nchi za
kusini mwa Afrika ni moja ya changamoto kubwa