Mkurugenzi tacaids ataka kondomu kugawiwa bure baa , gesti

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti
Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk Leonard Maboko ameeleza anavyotamani
kushuhudia Serikali ikigawa kondomu bure hasa katika maeneo hatarishi
ikiwemo 
nyumba zote wageni na kwenye baa.

Akizungumza leo Alhamisi Novemba 28, 2019 katika kongamano la kitaifa la maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani jijini Mwanza,Dkt. Maboko amesema ifike mahali hali ya kuzuia maambukizi isichukuliwe kama mzaha.
Amesema anatamani mwaka 2020 nyumba zote wageni, baa na maeneo mengine kondomu kugawiwa bure.
“Natamani mwakani tuweze kusambaza
kondomu kila mahali ili tuweze kudhibiti ugonjwa huu, najua huko ndiko
watu wanakutana na kufanya wanavyofanya lakini kama Serikali tuone
namna gani tunawasaidia wale wanaoshindwa kununua,” amesema Dk. Maboko

Amesema lengo ni kuzuia maambukizi mapya
ya Ukimwi kwa vijana kwa maelezo kuwa kwa sasa ndio kundi linaloongoza
kwa kupata maambukizi mapya.