Upembuzi yakinifu ujenzi wa reli ya kuunganisha tanzania na rwanda wakamilika

Tanzania
na Rwanda zinakamilisha mchakato wa ujenzi wa reli itakayounganisha
mataifa hayo mawili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).


Hayo yamesemwa  Jana Jumatano November 27, 2019 na Rais Magufuli wakati akizungumza na wananchi wa Isaka Mkoani Shinyanga.

“Nimeshazungumza
na Rais Kagame (Paul wa Rwanda) kuhusu utekelezaji wa mradi huu,
upembuzi yakinifu umekamilika. Kinachofanyika sasa ni kutafuta fedha,”
alisema Rais Magufuli.
 

Reli hiyo itakayounganishwa na ile ya kati itaanzia bandari kavu ya Isaka wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Mradi
huo ambao tayari hatua ya upembuzi yakinifu umekamilika utarahisisha
usafirishaji wa mizigo kutoka bandari kavu ya Isaka kwenda nchi jirani.