Brela yashiriki mkutano wa kikanda wa watalaamu wa masuala ya miliki bunifu afrika kusini

KAIMU Mkuu wa Kitengo cha Leseni za Biashara- (wanne kutoka kushoto) Tawi Kilumile ndiye Mwenyekiti wa Mkutano huo unaohusisha nchi 15 wanachama wa SADC Mkutano huo Tanzania imewakilishwa na Bakari Mketo Mkurugenzi wa Huduma na Uwezeshaji wa BRELA (wa kwanza kulia mstari wa pili)


Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni
(Brela) iliyopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara imeshiriki kwenye
Mkutano wa wa Kikanda Wataalamu wa masuala ya Miliki Bunifu kwa nchi za jumuiya
ya Maendeleo Kusini mwa  Africa (SADC) Johannesburg- Afrika Kusini
tarehe 25-26 Novemba, 2019.
Lengo la Mkutano huo ni Kuandaa Mpango kazi
wa Utekelezaji wa Mkakati (Framework) na Taratibu za kusimamia na kutumia
Miliki Bunifu katika Utekelezaji wa Mkakati wa Viwanda wa nchi wanachama wa
Jumuiya ya SADC.
Tanzania kwa Heshima iliyowekwa na Rais
ambaye ndiye Mwenyekiti wa SADC Bw. Mh Dr. John Pombe Joseph Magufuli Tanzania
imepewa heshima ya kuwa Mwenyekiti pia wa Mkutano huo
   

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni
-BRELA imewakilisha nchi katika Mkutano huo kwa kuwa ndiyo Ofisi ya Taifa ya
Miliki Bunifu (National IP Office)