Tcra yaendelea na kampeni ya mnada kwa mnada singida, wengi wajitokeza kujiandikisha na kusajili line

Mtoa wa huduma wa Kampuni ya Simu za Mkononi akimsajili mwananchi
kusajili laini ya simu kwa alama za vidole katika Kampeni ya Mnada kwa
Mnada iliyofanyika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya mabasi mkoani
Singida.
Wananchi wakiwa wamepanga foleni kwa ajili ya kuangalia namba ya
vitambulisho katika mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA
katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada iliyofanyika Viwanja vya Stendi ya
Zamani ya mabasi mkoani Singida.

Wananchi wakiwa katika vibanda vya watoa huduma za Simu Mkononi
kufanikisha usajili wa laini za Simu kwa alama za vidole katika Kampeni
ya Mnada kwa Mnada iliyofanyika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya mabasi
mkoani Singida
Mkuu wa Kanda ya Kati wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Anthony
Manyanda akizungumza na Wananchi wakati wa utoaji wa elimu ya usajili wa
laini za Simu kwa alama za vidole wakati wa Kampeni ya Mnada Kwa Mnada
iliyofanyika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya mabasi mkoani Singida.
Wakazi wa Mkoa  Singida na viunga vyake wamejitokeza kwa
wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi
Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA), Idara ya Uhamiaji  kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa
laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na
kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.
Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika Mikoa 18 lengo kuu ni nchi nzima kufikiwa na Kampeni hiyo.

 Mkuu
wa Kanda ya Kati  wa TCRA  Anthony Manyanda amesema ni fursa kwa
wananchi wa Mkoa Singida kufika Stendi ya zamani ya mabasi kwa ajili ya
kusajili kwa alama za vidole pamoja na kujiandikisha kupata usajili wa
vitambulisho vya Taifa  kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa
 mawasiliano. 

Manyanda
amesema kuwa  Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya
Wananchi kuhudumiwa hasa wakati huu usajili wa laini za simu kwa alama
za vidole pamoja Huduma zingine za mawasiliano..

Manyanda
 amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika  huduma  za simu
pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi na kuongeza kuwa muda
ni huu na kuacha kusubiri mwisho wa mwezi Desemba.

Amesema
 kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya
mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto
wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Manyanda
amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe
 wanapata ili waweze kusajili laini za simu kwa kwa  alama za vidole na
huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.

Hata hivyo amesema kuwa  kuna
watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi
Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kutoa elimu kuhusiana
 makosa ya jinai ya matumizi ya simu yasiofuata sheria.

Aidha
amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha
kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia
kitambulisho cha taifa.

Amesema  TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili watumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

Hata
hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za
vidole kabla ya  Desemba 31 na muda uliobakia ni mdogo tangu tangazo
lilipotolewa.

“TCRA
tutahakikisha tunawafikia katika wananchi katika utoaji wa elimu za
utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma
hiyo” amesema.Manyanda.

Manyanda amesema kuwa Kampeni hiyo imeanza kwa Mikoa yote iliyopo katika kanda ya Kati.
Nae
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa mwitikio
umekuwa mkubwa kwa Wananchi kutaka vitambulisho kwa ajili ya kusajili
laini za simu kwa alama za vidole.
Masasi amesema
kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA kupata elimu
na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika mamlaka husika
kupata vitambulisho.