Wafugaji kutumia simu kufuata malisho na maji

Mwandishi wetu,Monduli

Wafugaji 
wa wilayani tatu za mkoa wa Arusha,watakuwa wakifikia malisho na maji
ya mifugo yao kwa kutuma ujumbe wa simu kuulizia eneo lenye maji na
malisho na kujulishwa.
Rais wa Shirika la PCI Carrie Hetessler Radelet akizungumza  katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa kusasaidi wafugaji kuyafikia malisho na maji kwa kupitia huduma ya Afriscout wilayani Monduli
Kaimu Mkurugenzi wa PCI Jennifer Waugaman akiwa na mratibu wa PCI nchini John Laffa  wakipewa zawadi  baada ya kuzindua mradi huo

Mradi
huu umezinduliwa jana na shirika la  kimataifa la PCI ,l, katika kijiji
cha Arkaria wilayani Monduli na  utatekelezwa pia wilaya za Longido na
Ngorongoro ambazo zina idadi kubwa ya mifugo.

Akizungumza
katika uzinduzi huo, Rais wa PCI, Carrie Hetessler-Radelet alisema,
wafugaji kupitia simu zao za mkononi, baada yakupakuwa  application ya
Afriscout watatuma   bure ujumbe kwenda15054 kuuliza malisho na maji.

Hetessler –Radalet amesema baada ya kuuliza,mtandao huo utaonesha ramani za sehemu ya maji na malisho ambayo imepigwa angani.

Amesema
mradi huo, utawezesha wafugaji kuacha kusafiri muda mrefu kusaka
malisho, kuharibu mazingira lakini pia utapunguza vifo vya mifugo na
adha ya wafugaji kushindwa kufanya shughuli nyingine za kiuchumi.

Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo, Jennifer Waungaman amesema mradi huo ambao unatarajiwa kuwanufaisha sana wafugaji.

“tunawaomba wafugaji kutumia huduma hii ambayo pia itawasaidia kusimamia vizuri nyanda za malisho yao”alisena

Akizungumza
katika uzinduzi huo, Kaimu mkurugenzi endeshji wa malisho na vyakula
vya mifugo,Dk Asimwe Rwiguza  alisema mradi ho una manufaa makubwa kwa
wafugaji na amelitaka shirika hilo kupanua huduma hiyo nchi nzima.

Mfugaji
John Laizer amesema mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwao na
itaondoa tatizo la mifugo kufariki wakati wa kiangazi na migogoro na
wakulima.

Kaimu
Mkurugenzi halmashauri ya Monduli,Joseph Rutabingwa alisema halmashauri
ya Monduli itaupa ushirikiano mradi huo ili wafugaji wanufaike zaidi.

Mradi
huu pia unatekelezwa katika nchi tatu barani ambazo ni Tanzania, Kenya
na Ethiopia na shirika hilo linafanya kazi katika nchi 16 Duniani.