Breaking news: mwanamke atuhumiwa kumchinja mwanae na kumla nyama ludewa

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akiwa katika eneo la tukio yalipotokea mauaji ya Mama kumuua mtoto wake
Na Joctan Agustino, APC BLOG, NJOMBE
Mwanamke mmoja anaejulikana kwa jina la Christina
Mlelwa(38) pichani, mkazi wa Kijiji cha Mavanga kata ya Mavanga kitongoji Cha mji mwema
wilayani Ludewa mkoa wa Njombe anashikilikiwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za
kumchinja mwanae Joseph Gumbilo(4) mwenye ulemavu wa viungo na kumla nyama

Awali akizungumzia tukio hilo mkuu wa wilaya ya Ludewa
Andrew Tsere anasema mapema baada ya kufikishiwa taarifa za tukio hilo alilazimika
kufika eneo la tukio na kumhoji mtuhumiwa ambaye alikiri kutekeleza mauaji ya
mwanae na kisha kumkata viungo vyake  na
kumla na viungo vingine kuvitupa porini na chooni.

Tukio hilo linaleta mshituko kwa kamati ya ulinzi na usalama
mkoa na kumsukuma mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka kufika katika
kijiji hicho kuzungumza na wananchi na kisha kutoa agizo kwa wakuu wote wa  wilaya za mkoa huo kukamata kijiji kizima na
kuweka lockup endapo watagoma kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama
kuhusu matukio ya mauaji.

Katika hatua nyingine Olesendeka ameliagiza jeshi la polisi
kusaka ukweli wa tukio hilo haraka na wahusika kufikishwa mahakamani kama
ambavyo katiba inalinda haki ya kuishi ya kila binadamu bila kujali ulemavu
wake.

Katika mahojiano ya awali jeshi la polisi mama huyo ambaye
anaonekana kuwa na matatizo ya akili anakiri kuua na kukata vipande vipande na
kumla nyama huku masalia mengine ikiwemo fuvu la kichwa na miguu kutupa porini
hatua ambayo ililazimu kamati ya ulinzi kuvamia pori na kukuta vitu hivyo.

Mume wa Mwanamke huyo, Daniel Gumbilo anasema mke wake alisha wahi kufanya jaribio kama hilo miaka ya nyuma kwa mtoto wao mwingine
anaesoma lakini alishindwa baada ya majirani kumuwahi.

Nae kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa
anasema jeshi linaenda kuchunguza kwa kina zaidi kuhusiana na tukio hilo ili
wahusika wapewe haki yao ya hukumu ya uovu wao.


Kwa upande wa mtendaji wa kijiji cha
Mavanga Fadhiri Tajiri alisema ni kweli tukio hilo limetokea na kwamba taarifa
zaidi anasubiri muongozo kutoka kwa viongozi wake.


“Ni kweli Hilo tukio lipo
lakini viongozi wangu wamesema wapo njiani wanakuja nasubiri muongozo wa kutoka
kwao”alisema Tajiri.