Shehe wa Kijiji cha Mpwayungu Wilaya ya
Chamwino mkoani Dodoma, Nurdin Mbawala amesema watoto wa kike kuanzia
darasa la nne wanatumiwa na wazazi wao kuuza pombe za kienyeji hivyo
kuhatarisha usalama wao.

Aidha amesema hali hiyo inawaweka watoto hao katika hatari ya kutumika katika ngono wakiwa kwenye umri mdogo.
Akizungumza mwishoni mwa wiki katika
mkutano wa majadiliano kwenye mradi wa Sauti Yangu unaotekelezwa na
Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Woman Wake Up (Wowap), mradi
unaofadhiliwa na Shirika la Child Fund Korea kupitia Jukwaa la Haki za
watoto, alisema vitendo vya wazazi kupeleka watoto vilabuni
vimekithiripamoja na hatia zinazochukuliwa na serikali ya kijiji.

Alisema mtendaji wa kijiji hicho,
Selemani Kibakaya anafanya juhudi kubwa ikiwa ni pamoja na kutembea na
fimbo kuwasaka wanaofanya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto lakini
jambo hilo limekuwa likiendelea.

Alishauri viongozi wa vijiji kuweka mikakati kuhakikisha hakuna mtoto anayekwenda kilabuni kuuza pombe.
“Mtoto mdogo wa kike ndio maziwa
yanaanza kutoka tena yuko darasa la nne anashinda kilabuni kuuza pombe,
huyo mtoto anajengewa mazingira gani, usalama wake ukoje?” alisema.

Alisema wazazi wamekuwa wakitumia watoto kama mitaji na walevi ndio wanapenda kuhudumiwa na watoto kama hao.
“Huo ni ukatili wa hali ya juu sana,
hapo mzazi hawezi kuona shida kumuuza mtoto wake maana kuna watoto
walishaulizwa kwa nini wanauza pombe walisema mama zao waliwaambia kama
watakataa kufanya biashara hiyo hawataweza kununuliwa sare za shule au
madaftari.” Alisema.

Aliitaka jamii kulivalia njuga suala
hilo ili kuhakikisha watoto wa kike au hata wa kiume hawafanyi kazi ya
kuuza pombe kwenye vilabu.

Mwalimu Sane Nshashi wa shule ya Msingi
Nagulo Mwitikila alisema wakati wa kutungwa kwa sheria ndogo ndogo suala
la watoto kutumikishwa kwenye vilabu vya pombe za kienyeji liangaliwe
na kutungiwa sheria.

Alisema tatizo hilo limekuwa na athari
kubwa ka watoto wa kike kwani wanashinda vilabuni hadi usiku wa manane
na kukosa muda wa kujisomea na hata kupumzika.

Kwa upande wake Gabriel Hoya amesema
matatizo ya watoto yako mengi sio kwenye mimba tu hata suala la watoto
kutumikishwa kwenye vilabu vya pombe liangaliwe.

Pia alitaka kuangaliwa suala la wazazi
walevi ambao wamekuwa wakishinda na wakati mwingine kulala kwenye vilabu
vya pombe na kushindwa kutimiza wajibu wao kenye malezi ya watoto.

“Mzazi anashinda kilabuni, wakati
mwingine harudi nyumbani, watoto wanajilea wenyewe wanakwenda shule bila
viatu, mavazi yamechanika, hawajala hili ni tatizo kubwa.” amesema.

Akizungumza kwa niaba ya Ofisa Elimu wa
Kata, mwalimu Sunday Mtambo alisema pombe za kienyeji ni chanzo kikubwa
cha baadhi ya wazazi kutofanya kazi. /“Kuwe na muda maalumu wa kufungua
na kufunga vilabu ili pombe isilete athari kwenye uchumi wa familia,”
alisema.

Akijibu hoja hizo mtendaji wa kijiji cha
Mpwayungu, Selemani Kibakaya aliwataka wananchi kushirikiana ili
kuhakikisha watoto hawatumikishwi kwenye vilabu vya pombe za kienyeji.

Amesema sasa wamekuwa wakikamata watoto wanaotembea usiku, jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa watoto kuwa na woga.
Mratibu wa Wowap, Nasra Suleiman alisema jamii inatakiwa kushirikiana ili kulinda haki na ustawi wa watoto.