Rais
Magufuli amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NIDA kufika Mkoani Morogoro leo
na ikiwezekana akae Mkoani humo hata siku tatu ili kushughulikia tatizo
la Watu wengi kukosa vitambulisho vya Taifa huku Mkoa mzima ukiwa na
Ofisi moja pekee ya NIDA.
Mkurugenzi Mkuu NIDA afike hapa Morogoro ashughulikie hii changamoto ya
vitambulisho na nataka huduma hii iende kila Wilaya, haiwezekani Watu
wasafiri kutoka Wilayani kuja Mjini au muwape nauli na hela ya Gesti,na
hili litazamwe Nchi nzima Watu wapewe vitambulisho” amesema.
wanataka kusajili laini zao za simu na mambo mengine lakini zoezi la
vitambulisho linacheleweshwa na Watu wachache, suala la NIDA linaenda
polepole sana, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA nitahitaji unipe na tathmini ya
zoezi lote Nchi nzima”.
Aidha, Rais Magufuli amesisitiza kuwa katika kipindi chake cha uongozi hatopanga bei ya mkulima kuuza mazao yake.
“Wengine wanalalamikia bei ya mahindi kupanda, nataka wakulima
washangilie kama bei ya mahindi imepanda, biashara hii lazima iwe huru,
bei ya mahindi itajipanga yenyewe, wakati wa kuwapangia bei wakulima
kwenye mazao yao umekwisha,” amesema Rais Magufuli.