Tecmn wameipongeza mahakama ya rufaa ya tanzania kwa uamuzi wa kubatilisha kifungu namba 13 na 17 kwenye sheria ya ndoa ya mwaka 1971


Mratibu wa Mtandao TECMN,
Bw.Michael Singusia akiongea na Wanahabari katika Mkutano uliowahusisha
wadau mbalimbali wanaohusika na kuktetea haki za Mtoto nchini Baadhi ya wadau mbalimbali wa wanaohusika na utetezi wa haki za Mtoto nchini wakifuatilia mkutano 

NA EMMANUEL MBATILO


Mahakama katika shauri la Rebeca
Gyumi iliamuru Serikali kufanya marekebisho ya sheria ndani ya mwaka
mmoja na kusahihisha vifungu vya kibaguzi vya 13 na 17 na kuweka miaka
18 kama umri wa chini unaostahili kwa ndoa kwa wavulana na wasichana.


Ameyasema hayo leo Mratibu wa
Mtandao TECMN Bw.Michael Sungusia katika mkutano uliwakutanaisha wadau
mbalimbali kutoa tamko kutokomeza ndoa za utotoni Tanzania kupongeza
uamuzi wa Mahakama ya rufani ya Tanzania kuhusu mabadiliko ya sheria ya
ndoa 1971.


Akizungumza katika mkutano huo,
Bw.Sungusia amesema kuwa shauri la Rebeca Gyumi ni ushindi wa kipekee
kwa watoto wa kike wa Tanzania.Linaonesha kwamba wanawake wanapaswa kuwa
na haki ya kuridhia kuolewa na kwamba, umri wa chini wa kuolewa/kuoa
lazima uwe na miaka 18 kwa mwanamke na mwanaume.


“Shauri la Rebeca Gyumi dhidi ya
Mwanasheria Mkuu wa serikali katika shauri la madai Na.5 ya 2016
lilipinga uhalali wa kikatiba wa ndoa za utotoni.Matokeo yake ni kwamba
Mahakama Kuu Tanzania ilitamka kwamba vifungu vya 13 na 17 vya sheria ya
ndoa ni vya kibaguzi na vinakwenda kinyume na katiba”. Amesema
Bw.Sungusia.


Pamoja na hayo Bw.Singusia amesema
kuwa kwa wastani kati ya watoto watano wakike wawili huolewa kabla ya
umri wa miaka 18. Utafiti wa Kidemografia na afya (TDHS 2015)unaonesha
kuwa asilimia 31 ya wanawake kati ya umri wa miaka 20-24 waliolewa
wakiwa na umri wa chini ya m iaka 18.


Aidha, Bw.Singusia ameeleza kuwa
ndoa za utotoni kwa hapa Tanzania huathiri zaidi watoto wa kike kwani
kwa wastani wanawake wengi huolewa mapema zaidi kwa tofauti ya umri wa
miaka 5 wakilinganishwa na wanaume.