Mahakama
Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza imewahukumu kunyongwa hadi kufa
washtakiwa wanne kati ya saba waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya mauaji
ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza (RPC), Liberatus Barlow.

Hukumu
hiyo imetolewa jijini Mwanza jana Jumanne Novemba 12, 2019 na Jaji
Sirialus Matupa baada ya Mahakama kuridhika bila shaka yoyote na
ushahidi uliowasilishwa na washtakiwa walitenda kosa hilo.

Waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa ni Muganyizi Michael, Magige Mwita, Abdallah Petro na Abdulrahaman Ismail.
Walioachiwa
huru na Mahakama baada ya ushahidi kutowatia hatiani katika kesi hiyo
ya mauaji namba 192/2014 ni Chacha Mwita, Buganizi Edward na Bhoke
Marwa.

Kamanda
Barlow aliuawa kwa kupigwa risasi katika tukio lililotokea eneo la
Kitangiri Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza saa 8:00 usiku wa kuamkia
Oktoba 13, 2012.