NA; MWANDISHI WETU
Serikali
ya Awamu ya Tano imedhamiria kuendelea kutatua changamoto zinazoikabili
sekta ya usafirishaji hapa nchini ili iweze kuongeza mchango wake
katika kukuza uchumi.

Akizungumza Novemba 1, 2019 Jijini Dodoma wakati wa mkutano wa pamoja
kati ya Vyama vya Madereva na Vyama vya Wamiliki wa Vyombo vya
Usafirishaji, Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kujenga mazingira
wezeshi kati ya wadau wote wa sekta ya usafirishaji hapa nchini wakiwemo
madereva na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji.

“Moja ya maazimio ya mkutano wetu wa leo ni kuwataka wamiliki wa vyombo
vya usafiri ambao hawajatoa mikata ya ajira kwa madereva wao waanze
kutoa mikataba ya ajira iliyoboreshwa suala hilo lianze kutekelezwa mara
moja kwa kuwa ni takwa la kisheria na sio jambo la hiari” Alisisitiza
Mhagama

Kutolewa kwa mikataba hiyo ni matokeo ya makubaliano yaliyofikiwa kati
ya pande hizo mwaka 2017 yakitaka kuwepo kwa mikataba ya ajira
iliyoboreshwa kwa madereva wote itakayoleta ustawi wa maslahi ya pande
hizo na Taifa kwa ujumla.

Alifafanua kuwa mkutano huo umefanikisha kufikiwa kwa maazimio ya pamoja
kati ya Serikali, wamiliki na madereva kupitia viongozi wa makundi hayo
ili kuchochea ustawi wa sekta hiyo na kuondoa hali ya malalamiko na
mapungufu yaliyobainika katika ukaguzi uliofanyika mwezi Julai na Agosti
2019 kwa lengo la kuona namna sheria za kazi zinavyozingatiwa.

Azimio jingine ni kuendelea kutoa elimu kwa makundi hayo kupitia vyama
vya wamiliki na madereva ili kupunguza au kuondoa changamoto zilizopo
hasa zilizoibuliwa katika ukaguzi uliofanyika hivi karibuni.

Aidha, Waziri Mhagama ameviagiza vyama vya wamiliki wa vyombo vya
usafirishaji kuhakikisha wanaruhusu wafanyakazi kuanzisha matawi ya
vyama vya wafanyakazi kwa Makapuni ambayo hayajafanya hivyo bado.

“Vyama vya wafanyakazi vinasaidia sana kuleta tija na ufanisi katika
maeneo ya kazi maana wafanyakazi hutumia vyombo hivyo kushauriana namna
bora ya kutatua changamoto zinazowakabili,” alisema Mhagama

Katika hatua nyingine Waziri Mhagama aliwataka madereva na wamiliki wa
vyombo hivyo kuendelea kuzingatia sheria na kuthamini utu na heshima
pande zote mbili, Serikali itachukua hatua kwa yeyote atakayekiuka
misingi hiyo.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Vijna na Ajira
Mhe. Antony Mavunde amesema kuwa maazimio yaliyofikiwa katika mkutano
huo yatasaidia kutatua changamoto zilizoibuliwa na madereva na wamiliki
wa vyombo vya usafirishaji.

Mkutano wa wadau wa sekta ya usafirishaji umefanyika Jijini Dodoma
ukishirikisha Wizara zinazohusika na masuala ya uckuzi na Ujenzi.