Na Beatrice Mosses – Manyara
Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amempa mtihani mkandarasi wa
kampuni Mkandalasi Gopro construction Ltd, anayetengeneza barabara ya
Mbulu mjini kwa kiwango cha lami.
Mnyeti amemwambia mkandarasi huyo kuwa iwapo kama atafaulu mtihani wa
kutengeneza barabara hiyo ya mita 500 alizopewa kwa kiwango
kinachotakiwa yupo tayari kumpa km. 05 zinazotakiwa kutengenezwa mjini
hapo ambazo ziliahidiwa na Rais Magufuli.
Mnyeti ameyasema hayo wakati alipokuwa akikagua barabara hiyo ya mita
500 za mwanzo ambapo kwa sasa ujenzi wake bado unaendelea.
“Hakikisheni mnamaliza huu mradi mapema na kwa wakati ili niweze
kuwaletea fedha zingine sio mradi unakaa, mnakaa, tunaombea fedha
zinakuja halafu zinakaa bila kazi inakuwa hakuna mnachokifanya.
“Sasa tengenezeni kwa kiwango ili mpate kazi nyingine, mkiharibu mimi
sitakubali mpate tenda nyingine, mnaweza mkaenda pale Babati yule
mkandarasi amefanya kazi ya hatari sana na ndio maana tumemuongeza kazi
nyingine.
“Na nimeagiza TARURA wampe ile lami yote mpaka amalize hata kama watu
watakuwa wanalalamika sijui tenda zimekiukwa ni kwa sababu kiwango
anachotengeneza pale ni cha kiwango cha juu sana.
“Sasa bwana mzee tunakupa mtihani huu wa kwanza mita 500 ukitekeleza kwa
kiwango cha juu hata tenda hatutatangaza kwa sababu sisi tunataka ubora
na hapa kuna km 05 na pesa ipo sisi ni namna tu mnaitumiaje kwa haraka
na kwa spidi inayotakiwa”, alieleza Mnyeti.
kiwango cha juu hata tenda hatutatangaza kwa sababu sisi tunataka ubora
na hapa kuna km 05 na pesa ipo sisi ni namna tu mnaitumiaje kwa haraka
na kwa spidi inayotakiwa”, alieleza Mnyeti.