Tcra kampeni ya mnada kwa mnada nyehunge wilayani sengerema katika utoaji wa elimu ya usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole

Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam 
Kampeni ya Mnada kwa Mnada imeanza 0ktoba 11 katika
maeneo Kome Pamoja Maisome kwa siku mbilimbili  ikiwa ni kuwafikia
wananchi wengi katika wilaya hiyo.
Akizungumza
katika Kampeni ya  Mnada kwa Mnada katika Viwanja vya Nyehunge Wilayani
Sengerema Mkuu wa Kanda Ziwa  Mhandisi Francis Mihayo amesema
wamejipanga kuwafikia wananchi wote wawemejisajili laini za simu kwa
alama za vidole.

Wananchi wakipata huduma ya Usajili wa Vitambulisho vya Taifa katika Viwanja Nyahunge

Mhandisi
Mihayo amesema katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa NIDA wapo katika kusajili wananchi vitambulisho
kwa ajili ya kufanya Usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.


Mhandisi Francis Mihayo akizungumza na wananchi wakati wa Kampeni ya
Mnada kwa Mnada uliofanyika katika Viwanja vya Nyehunge Sengerema
Wananchi wakisoma vitabu vya muongozo wa TCRA katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Nyehunge Sengerema.

Wakazi
wa Nyehunge Wilayani Sengerema na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi
katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi
Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA), Idara ya Uhamiaji  kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa
laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na
kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.


Kampeni
tangu imeanzishwa imekwenda katika Mikoa 16 lengo kuu ni nchi nzima
kufiwa na Kampeni hiyo katika kuwawezesha wananchi kupata elimu ya
Mawasiliano Pamoja usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Amesema
ni fursa kwa wananchi wa Sengerema kujitokeza kujisajili laini za simu
kwa alama za vidole na  huduma nyinginezo  kutokana  na kuwepo kwa
mnyororo   wadau wa  mawasiliano. 

Aidha
Mihayo  amesema kuwa  Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa
ya Wananchi kuhudumiwa hasa wakati huu usajili wa laini za simu kwa
alama za vidole ili wasiweze kumuacha mtu yeyote kutotumia simu ifikapo
Desemba 31 mwaka huu.

Amesema
muda uliopo ni miezi mitatu hivyo Wananchi wakamilishe taarifa
zinazohitajika katika kujisajili laini za simu  kwa alama  za vidole ili
kuondoa usumbufu mwisho wa Desemba kwa watu kupanga foleni.

Mhandisi
Mihayo amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika mawasiliano ya
simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi.

Amesema
 kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya
mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto
wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Amesema
kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi
Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kuwaelewesha makosa
ya jinai ya matumizi ya simu.
Aidha amesema Kampeni
hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi
anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha
taifa cha NIDA.

Mhandisi
Mihayo amesema kuwa TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili
mtumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

“TCRA
tupo tayari  kuwafikia  wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa
bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo” amesema
Mhandisi Mihayo.

Nae
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa mwitikio
umekuwa mkubwa kwa Wananchi kutaka vitambulisho kwa ajili ya kusajili
laini za simu kwa alama za vidole hali na kufanya wananchi wengi
wamepata vitambulisho vya Taifa na kusajili laini za simu kwa alama za
vidole.

Masasi amesema
 Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA kupata elimu na
baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika mamlaka husika kupata
vitambulisho.

Ameongeza kuwa watahakikisha kila mwananchi anajisajili kwa alama za vidole kwani Watu wana haki ya kuwa na mawasiliano ya simu