Lusinde: kijana mdogo,una miaka 22,huna kazi ya uhakika,huna mshahara lakini una mademu wanne ,wewe ni tatizo


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Mbunge
wa jimbo  la Mtera mkoani Dodoma Livingstone Lusinde amewataka vijana
kote nchini kujitathimini na kuachana na masuala ya anasa ikiwa ni
pamoja na Umalaya na badala yake wawajibike katika kazi za kuwaletea
maendeleo. 


Mhe.Lusinde
amesema hayo jijini Dodoma akiwa mgeni Rasmi katika kongamano la 
Vijana Mkoa wa Dodoma lililolenga kujadili mchango wa  Baba wa Taifa
Mwl.Julus  Kambarage Nyerere ikiwa  taifa la Tanzania likifanya
kumbukizi ya Miaka 20 tangu afariki dunia  mwaka 1999. 



Mbunge
huyo amesema vijana wa siku hizi wamekuwa wakifanya masuala ya Umalaya
na ukahaba na mambo mengine ya anasa wakiwa wadogo na kushinda baa
badala ya kuwajibika katika kazi hivyo wanapaswa kubadilika. 



“Kijana
Mdogo,una miaka 22,huna kazi ya uhakika,huna mshahara lakini una mademu
wanne ,wewe ni tatizo,shida ni wewe,piga hela zote ulizotoa Guest na
chipsi ni mtaji.Wewe ni tatizo kubwa,huwa ninaangalia sana mitaala ya
elimu,wakati mwingine watoto tunawafundisha ujinga.Alisema. 



Mhe.Lusinde
amesema kuna baadhi ya mambo vijana wanatakiwa kujitathimin na kufanya
mambo makubwa na kwa kasi na kuacha kupoteza muda kupoteza fedha kwa
kujiunga internet na kuchati kwenye Magroup ya Whatsaap yasiyokuwa na
tija kwani ni kupoteza muda na badala yake watumie miundombinu
iliyoachwa na   Mwalimu Nyerere katika kuwaletea Maendeleo. 



“Lazima
kuna baadhi ya vitu unapaswa kugundua na kung’amua,lazima miundombinu
tuifanyie kazi katika kutuletea maendeleo,kuna mambo mengine yanahitaji
haraka,mtu anakwambia polepole ndio mwendo na wewe unakubali.huna
shughuli,huna mshahara lakini una simu tatu unachati group hili hadi
lile,wewe ni Poyoyo.Amesema. 



Hata
hivyo,Mhe.Lusinde amewaasa  Vijana kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere kwa kupambana na rushwa kwani rushwa hunyonya
haki ya mtu. 



Aidha,Mhe.Lusinde
amewataka vijana kujiandaa mapema pindi wanapotaka kufanya maendeleo na
akatolea mfano mwanafunzi anayefaulu vizuri mtihani ni Yule
aliyejiandaa mapema katika  na kudai kuwa ng’ombe hanenepi siku ya
mnada. 



Kwa
upande wake katibu wa  Vijana mkoa wa Dodoma Joel Makwaia  amesema
Mwl.Nyerere alikuwa kiongozi Mzalendo wa Taifa na alijitolea kwa hali na
mali ili kuhakikisha taifa linasonga mbele.