“wapinzani ni wadudu” asema mbunge wa chama tawala tanzania

Mbunge
wa chama tawala nchini Tanzania, Rashidi Chuachua wa jimbo la masasi mjini
amewataka wananchi wa jimbo hilo kutowachagua viongozi wa vyama vya upinzani
kwa kuwa hao ni wadudu.
 


“Sisi
kama CCM hatupo tayari kufanya kazi na wadudu, msituletee wadudu. Na hii
wairekodi, mimi nawaita wadudu. Tunataka kufanya kazi na watu ambao wako tayari
kujenga nchi na sio majungu na midomo,” alisema mbunge Chuachua.

Kauli
hiyo ambayo imezua gumzo katika mtandao na kufananishwa na kile kilichotokea
katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda kwa sababu kuna watu waliokuwa wanawaita
wenzao mende.

Hivyo
kutafsiriwa kama uchochezi.

Wanasheria
maarufu nchini humo, Fatuma Karume na Jebra Kambole wamevuta mjadala mkali
kutoka kwa watu ambao wanahoji , wadudu ina maana gani?

Katika
mjadala huo, wengine wanahoji kuhusu hao wanaopiga makofi kwa kumshangilia, je
kile wanachopigia makofi wanafurahishwa nacho au hawakuelewa maana yake.
 

Mchambuzi
wa masuala ya siasa Mohamed Issa, anasema kuwa nafasi ya mbunge katika jamii ni
kubwa sana na lugha ambazo kiongozi huyo anatumia zinaweza kumfanya akose
nafasi ya ushindi.

“Hafai
kuwa kiongozi, lugha ndio dhamana ya kiongozi” amesema Mohamed Issa.

Aliongeza
kusema kuwa “Hizo sio lugha za kusikika kutoka kwa viongozi,

Kile
kilichotokea nchi ya jirani ya Rwanda ni mafunzo tosha”. Mohamed Issa
alisisitiza.

Kauli
hiyo ya wapinzani kuitwa wadudu imetamka wakati ambao wananchi wa taifa hilo
wamekuwa na muitikio mdogo wa kujiandikisha kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi
wa viongozi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24.
 

Aidha
mbunge huyo alitoa ufafanuzi wa kauli yake.

“Hiyo
itakuwa tafsiri zao tu. Mimi ni mwanasiasa nimetamka nikiwa kazini. Nimesema
binadamu kamili ana utashi, issue yangu ni kwamba kila mtu anaona tunachofanya.
Mwenye utashi anaweza kufafanua, akakosoa,” Chuachua aliliambia gazeti la
Mwanachi jana.

“Asiye
na utashi hawezi kuona zuri wala baya. Hata mdudu hajui zuri wala baya. Kwa
hiyo watu wanaweza kutumia tafsiri hii kwa namna wanavyotaka wao”.