Rais magufuli aaahidi kuendelea kumuenzi mwalimu nyerereRais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
kwenye sherehe za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi
ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika Uwanja wa
Michezo wa Ilulu Mjini Lindi Oktoba 14, 2019

**
Rais 
Magufuli ameahidi kuwa serikali ya awamu ya tano itaendelea kumuenzi
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere bila uoga wowote kwa kutekeleza
mambo mbalimbali ambayo alitamani kuyafanya enzi za uhai wake.


Ametoa
ahadi hiyo leo Jumatatu Oktoba 14, alipokuwa akihutubia wananchi katika
hafla ya maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge wa uhuru, kumbukizi
ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na wiki ya vijana kitaifa
inayofanyika katika uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi.

“Serikali
ninayoingoza itaendelea kumuenzi Baba wa Taifa, kuheshimu tunu za
mwenge pamoja kuendelea kuwathamini vijana ikiwemo kuwateua kushika
nafasi mbalimbali za uongozi na wito wangu kwa vijana watakaoteuliwa
kushika nafasi hizo wajitahidi kufanya kazi kwa bidii na uzalendo
mkubwa,”.

“Tumejitajidi
kumenzi Baba wa Taifa kwa kupambana na vitendo vya rushwa, wizi,
ubadhilifu wa mali za umma mambo ambayo aliyachukua enzi za uhai wake na
katika hilo tumeanzisha kitengo maalumu cha mahakama cha kushugulikia
mafisadi pia tumeondoa watumishi hewa takribani 20,000 na wafanyakazi
wenye vyeti vya kughushi takribani 14,000,”

“Ili
kuendelea kuenzi mchango mkubwa uliotolewa na Baba wa Taifa hatuna budi
kuwafundisha vijana wetu kuhusu mambo muhimu ambayo yalisimamiwa na
baba wa Taifa katika uhai wake ikiwemo uzalendo, uaminifu, nidhamu,
uchapakazi na moyo wa kujitolea kwani tusipofanya hivyo tutakuwa
tumeliangamiza taifa letu kwasababu vijana ni kundi kubwa na ndio
viongozi wa leo na kesho,” amesema Rais Magufuli.

Aidha
amewataka Watanzania kumuishi Mwalimu Nyerere kwa kutimiza maono yake
aliyotamani kuyatimiza, kusimamia miiko ya azimio la Arusha pamoja na
kudumisha umoja bila kubaguana kwa dini waka kabila.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *