Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Mhe.Paul Makonda ameelekeza Watumishi wa TAMISEMI wanaohusika na Miradi
ya ujenzi wa Mifereji na Mito kupitia DMDP kuhakikisha kabla ya October
10 mwaka huu miradi yote ya Ujenzi wa Mifereji Wilaya ya Ilala iwe
imeanza na endepo watakaidi atahitisha maandamano ya wakazi wa Kata 5
kwenda Wizara ya TAMISEMI.

RC Makonda ametoa maagizo hayo
baada ya kutembelea Mfereji wa Kisiwani kata ya Buguruni ambao tangu
mwezi May mwaka huu aliagiza ufanyiwe maboresho kutokana na mfereji huo
kuwa chanzo cha mafuriko kwenye makazi ya watu lakini ameshangazwa kuona
hadi leo anafika site anakuta hakuna chochote kilichofanyika licha ya
mkataba kusainiwa tokea mwezi wa Saba mwaka huu.

Jambo hilo lilimlazimu RC Makonda
kumpigia simu Mratibu wa Miradi ya DMDP Bwana Emmanuel Ndyamkana ambae
alijitetea kuwa miradi hiyo inakwama kutokana na wizara ya fedha
kuchelewa kutoa fedha jambo ambalo RC Makonda amesema ni uzembe.

Aidha RC Makonda ameitaja baadhi
ya Mifereji na Mito inayotakiwa kufanyiwa maboresho ni pamoja Mfereji wa
Tabata kanisa la Roman catholic, mfereji wa Kiwalani na baadhi ya Mito
yenye urefu wa Km 19 ambayo ujenzi wake utagharimu takribani Shilingi
Bilioni 32.

Pamoja na hayo RC Makonda
ametembelea Mradi wa Ujenzi wa Machinjio mpya ya Vingunguti na
kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo ambapo amewataka NHC kuhakikisha
ujezni unakamilika kwa muda uliopangwa.