Kimbunga chasababisha maafa arusha

Na Lucas Myovela_Arusha.

Kufuatia
kimbinga kilichotokea tarehe 01 octoba jijini Arusha kinasadikika
kusabibisha maafa makubwa ikiwemo kuzama kwa mitumbwi miwili ya kitalii
katika ziwa Momela liliopo katika hifadhi ya Taifa ya Arusha ( ANAPA ) 
wiliyani Arumeru mkoani Arusha.

Katika
tukio hilo la kuzama kwa mitumbwi miwili iliyokuwa imebeba watalii
kutoka nchini Ujerumani kunusulika kifo baada ya mitwimbwi hiyo kuzama
pamoja na muongoza watalii kutoka kampuni ya kitalii ya Wayo Africa
aliyejulikana kwa jina la Samwel Gildati Mhina anayefanya kazi na
kampuni ya kitalii ya Wayo Africa kutoonekana mpaka sasa huku zoezi la
kuendelea kumtafuta likiendelea katika ziwa hilo.
Akithibitisha
tukio hilo kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ACP Koka Mhita
amesema kuwa toka jana majira ya saa 8:45 mchana kimbunga kikubwa
kilitokea katika kitongoji cha Momela katika kata ya Ngalenanyuki
wilayani Arumeru na kuzamisha mitumbwi miwili iliyokuwa imebeba watalii
wawili raia wa ujerumani waliyokuwa wakiendelea na utalii ndani ya ziwa
Momela ndipo walipo kutwa na dhahama hiyo.
Kamanda
amesema kuwa watu watatu kati ya wanne wameweza kuokolewa ambao ni
watalii wawili na muongiza watalii mmoja waliyokuwa ndani ya mitwimbwi
hiyo  huku akiwataja kwa majina watalii hao ni Dr Rosenberger pamoja na
mumewe Dr Tuemper Bern John wote raia wa ujerumani waliyoweza kuokolewa
baada ya jitihada zao za awali za kutaka kujiokoa kuzaa matunda pamoja
na muongoza utalii mmoja aliyefamika kwa jina la Yona Mosha.
Na
kuongeza kuwa mpaka sasa muongoza watalii mmoja Bw Samwel Mhina (29)
bado hajapatikana pamoja na mtumbwi wake huku jitihada za ukoaji kutoka
katika kikosi cha zima moto mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na jeshi la
polisi mkoa wa Arusha na wilaya ya arumeru zikiendelea na kazi hiyo ya
kumtafuta ambapo mpaka hivi sasa bado hajapatikana.
Pia
kamanda ameeleza kuwa mbali na kimbunga hicho kuzamisha mitumbwi miwili
pia kimeweza kuleta maafa makubwa kwa wananchi kwa kuaribu nyumba za
makazi,nyumba za ibada paomja na miundombinu hasa miundo mbinu ya umeme.
MADHARA YA KIMBUNGA KATIKA MIUNDOMBINU YA TANESCO.
Akitoa
taarifa za kuharibiwa kwa miundombinu ya umeme katika jiji la Arusha
Mhandisi mkuu wa shirika hilo mkoani hapa Ronesiano Shamba ameeleza kuwa
miti mikubwa iliyoanguka baadabya kung’olewa na na upepo mkubwa huo
kutoka umbali wa zaidi ya mita nane hadi kutupwa katika nyaza za umeme
katika maeneo mbali mbali katika jiji la Arusha.
Akitaja
maeneo yaliyokubwa na uharibifu huo mkubwa huo wa miundombinu ya umeme
ni wilaya ya Monduli yote,kata ya olasiti,Sombetini,Iliboru,Sokoni one,Kimandolu,Moivo,Moshono,Kijenge
kwa maeneo ya jiji la Arusha pamoja na halmashauri moja ya Monduli
ambayo yenyewe iliathira yote na mpaka sasa jitihada za kurudisha umeme
zikiendelea.
Pia katika
halmashauri ya Arumeru ni katika maeneo ya Kata ya Kikwe,Patandi pamoja
na Usa River,huku garama zote za miuondombinu iliyo haribika  zikielezwa
kuwa zaidi ya shilingi milioni 400 mpaka sasa huku bado tathimini
nyingine zikiendelea kufanyika.
Mbali
na kimbunga hicho kuleta madhara makubwa hayo bado shirika la umeme
Tanesco Jiji la Arusha linaendelea na jitihada za kurudisha umeme kwa
maeneo ambayo bado hayapata umeme kutokana na athari hizo pia
kuhakikisha wananchi wanaendelea na shughuli zao kwa uhakika na
kwausalama pasipi madhara yeyote yale yatokanayo na umeme.

Pia
Mhandisi Shamba amewataka wakazi wa jiji la Arusha kuondoa hofu juu ya
shirika hilo la Tanesco na kuto kugusa nyaya za umeme zilizo anguka
chini na kuwataka watoe taarifa mara moja pindi wainapo tofauti yeyote
ya miundo mbinu ya umeme