Tazama hapa mkuu wa wilaya ya kisarawe jokate mwegelo alivyobadilisha maisha ya huyu mama

Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ametimiza ahadi yake kwa Mama wa
Mapacha kwa kumjengea nyumba yakuishi baada ya ile ya awali iliyokuwa
haina mazingira mazuri ya kuishi, Jokate amesema watamkabidhi mama huyo
nyumba hiyo ambayo inavyumba viwii vyenye tiles, umeme, choo, jiko na
mahitaji mengine ya msingi.


Kupitia
ukurasa wake wa  facebook DC Jokate ameshare habari hiyo kwa
kuambatanisha muonekano wa picha za nyumba ya awali na ya sasa
aliyomjengea kwa kushirikiana na baadhi ya makampuni waliojitolea.

”Naomba
Mungu aendelee kututumia sisi viongozi na watumishi wake kuweza kugusa
na kubadilisha maisha ya watu wengi zaidi. Tujitoe zaidi kuliko
kufikiria maslahi yetu binafsi. Hatimaye ahadi tuliyotoa kwa mama wa
mapacha waliotenganishwa Muhimbili imetimia. Na leo tunaenda kumkabidhi
nyumba mpya ya kisasa ya vyumba viwili yenye tiles, umeme, choo, jiko na
mahitaji mengine ya msingi. Ukilinganisha na nyumba ya awali aliyokuwa
akiishi ya makuti kule Kimalamisale.

“Kipekee
nawashukuru ubatanzania kwa kushirikiana na Ofisi Ya Mkuu Wa Wilaya
kusimamia ujenzi kwa kutoa fedha za ujenzi na
africanreflectionsfoundation kwa kushirikiana na Ofisi Ya Mkuu Wa Wilaya
katika kununua kiwanja. Kwahiyo nyumba na kiwanja ina hati yenye majina
ya watoto mapacha. Nimshukuru pia Michael Afisa Tarafa Mzenga kwa
kusimamia vizuri ujenzi na mafundi wote walioshiriki. .Tukutane Mzenga
leo kwenye makabidhiano.”  Ameandika Jokate