Ofisi ya makamu wa rais yaadhimisha siku ya tabaka la ozoni…

Kaimu
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira kuutoka Ofisi ya Makamu wa 
Rais, Bi Kemilembe Mutasa akiongea na Mafundi wanaohudumia gesi za
majokofu na viyoyozi wakati wa warsha ya mafunzo kuadhimisha  siku ya
tabaka la ozoni Duniani iliyofanyika katika Chuo cha Ufundi Stadi (VETA)
Chang;ombe jijini Dar E s Salaam.
Mgeni
Rasmi katika Warsha ya siku moja ya maaadhimisho ya siku ya ozone
Duniani Bibi  Vaileth Fumbo akiongea na Washiriki wa warsha hiyo ambayo
ilifanyika katika Chuo cha VETA jijini Dar Es Salaam. Washiriki wa
warsha hiyo ni Mafundi wa gesi za majokofu na viyoyozi
Sehemu
ya Washiriki wa warsha ya mafunzo ya maadhimisho ya siku ya ozoni
Duniani wakimskiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani) warsha hiyo ilifanyika
katika Chuo cha mafunzo ya  Ufundi –VETA Chang’ombe
Washiriki
wa warsha hiyo wakipatiwa mafunzo juu ya utunzaji wa gesi iliyotolewa
kwenye jokofu na baadaye kuweza kutumiwa tena (badala ya kuacha isambae
hewani na kuharibu tabaka la hewa). Gesi hiyo inatunzwa na kifaa
kiitwacho recovering unit.

Utafiti wa kisayansi katika tabaka
la ozoni katika karne ya ishirini ulithibitisha kumong’onyoka kwa 
tabaka hilo kutokana na kulundikana angani kwa kemikali aina ya chloroflourocarbons (CFCs), halons, methyl choroform, methyl bromide, carbon tertrachoridena nyinginezo. 

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo cha VETA– Chang’ombe Bi Vaileth Mfumbwa
wakati wa warsha ya mafunzo kwa Mafundi mchundo wanaoshughulikia
majokofu na viyoyozi  ikiwa ni maadhimisho ya siku ya tabaka la ozoni
Duniani iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, iliyofanyika katika
Chuo cha VETA-Chang’ombe jijini Dar Es Salaam.

Aliongeza kuwa Kemikali hizi
hutumika katika majokofu, viyoyozi, vifaa vya kuzimia moto, ushafishaji
chuma, utengenezaji wa magodoro, madawa na manukato ya kupulizia,
ufukizaji wa udongo katika vitalu vya tumbaku na mashamba ya maua na
ufukizaji wa mazao katika maghala kabla ya kusafirishwa nje ya nchi.
Matumizi ya kemikali hizi yapo kwa wingi katika nchi zilizoendelea na
zinazoendelea, kama Tanzania.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi, Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Mazingira Bi Kemilembe Mutasa  alisema kuwa ,
Kitaifa maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya
Tabaka la Ozoni yanafanyika jijini Dar es Salaam ambapo Ofisi ya Makamu
wa Rais – Muungano na Mazingira kwa kushirikiana na Wakufunzi wa Chuo
cha Ufundi Dar es salaam wamepanga kutoa mafunzo kwa vitendo kwa mafundi
mchundo wanaohudumia majokofu na viyoyozi kuhusu njia bora za kuhudumia
vifaa hivyo; kutoa elimu jinsi ya kutumia vitambuzi vya gesi; na
kubadilisha tekinolojia zinazotumia kemikali haribifu kwa tabaka la
Ozoni kwa kemikali mbadala.

“Katika maadhimisho haya,
tunakumbushwa kuwa katika Mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa
Monteral uliofanyika nchini Rwanda mwaka 2016, nchi wanachama
zilikubaliana kupunguza uzalishaji na utumiaji wa  kemikali jamii ya Hydrofluorocarbons (HFCs)
ambazo pia hujulikana kama R-143a kwa jina la biashara  na kukubaliana
kuzuia ongezeko la joto la dunia kwa nyuzi joto 0.5 (0.5 degrees
Celsius)” alisema Bi. Mutasa


Warsha hiyo ya mafunzo ya siku
moja imekua chachu kwa Mafundi Mchundo wanaoshughulikia majokofu na
viyoyozi kwa kufundishwa njia mbalimbali za kiutaalamu za kutumia
wanapokua katika shughuli zao za kila siku.  Mafunzo hayo yalitolewa na
Wakufunzi wa Chuo cha Ufundi-VETA Chang’ombe jijini Dar Es Salaam.