Dhana ya afya moja yaanza kutekelezwa kwa vitendo mpakani namanga

Tweet on Twitter

Na. Mwandishi Wetu, APC BLOG Namanga

Tanzania kwa kushirikiana na Kenya jana tarehe 11 Juni, 2019, wameanza kutekeleza zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, lilofunguliwa jana mpakani mwa Tanzania na Kenya kwenye eneo la Namanga.
Zoezi hilo, linazingatia Dhana ya Afya moja ambayo hujumuisha sekta ya afya ya binadamu, wanyamapori, mifugo na mazingira katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu. Wataalamu wa sekta hizo leo tarehe 12, Juni, 2019, wameendelea kutekeleza zoezi hilo kwa kuzingatia Dhana hiyo.
Wataalamu wa sekta za Afya wa Tanzanaia na Kenya, katika makundi tofauti wameweza kutekeleza kwa vitendo kwa kutumia Dhana ya Afya moja katika kuhakiki matumizi ya maabara zinazohamishika, kutathmini uwezo wa uchunguzi na usimamizi wa wagonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa mpakani, pamoja na kufanyia majaribio ya utekelezaji wa Mipango ya Dharura ya Taifa na Kanda, Miongozo ya Utendaji katika kukabili na kupunguza madhara ya Bonde la Homa ya Ufa kwa Wanyama na Binadamu.