Tetesi za soka ulaya alhamisi 22/08/2019: sancho, nyemar, havertz, wanyama, almada


Ombi la Barcelona la kumnunua kwa mkopo wa dau la £137m pamoja na kumpatia kandarasi ya kudumu mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27, limekataliwa na PSG huku mabingwa hao wa ligue 1 wakiitisha dau la £229m. (Marca)

Manchester United imemfanya winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 19, lengo lao kubwa katika uhamisho wa mwezi Januari na wanajiandaa kutoa dau la £100m. (Sun) 
Haki miliki ya pichaTF-IMAGES
Liverpool, Manchester City, Manchester United, Arsenal na Chelsea ni miongoni mwa klabu kuu barani Ulaya zinazomlenga mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 20, ambaye ana thamani ya £91m. (Sport1 – in German)


Beki wa Liverpool na raia wa Croatia asiyehitajika sana Dejan Lovren, 30, anaivutia klabu ya Ujerumani ya Bayer Leverkusen baada ya kufeli kupata uhamisho kuelekea Roma. (Bild – in German)
ottenham imeanza mazungumzo ya kumuuza kiungo wa kati wa Kenya Victor Wanyama, 28, kuelekea klabu ya Bruges kwa dau la £11m.


Mshambuliaji wa Ubelgiji Michy Batshuayi, 25, anataka kusalia na kupigania nafasi yake Chelsea lakini ataitazama hali mwezi Januari. (Standard)

Manchester City inachunguza hali ya kiungo wa kati wa Argentina na klabu ya Velez Sarsfield Argentine Thiago Almada, 18, ambaye bado hajaandikisha upya kandarasi yake na klabu hiyo.. (A Bola, via Manchester Evening News)


Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anataka kiungo wa kati wa England Herbie Kane, 20, kushiriki katika mechi yao ya kombe la Carabao Cup na hivyobasi kumaliza matumaini ya Portsmouth, Sunderland na Coventry kumsaini mchezaji huyo kwa mkopo. (Portsmouth News)


Bayern Munich inamuuza beki wa Ujerumani Jerome Boateng, 30,kwa dau la £22m. (Mail via Marca)


TETESI ZA SOKA JUMATANO





Mchezaji mpya wa Real Madrid Real Luka Jovic huenda akajiunga na AC Milan kwa mkopo miezi miwili tu baada ya mshambuliaji huyo ,mwenye umri wa miaka 21 kukamilisha uhamisho wa dau la £62m kuelekea katika klabu hiyo ya Uhispania. (Gazzetta, via Sport Bible)


Klabu ya Uturuki ya Fenerbahce inataka kumsaini beki wa Manchester United na Argentine Marcos Rojo, 29, kwa mkopo . (A Spor, via Manchester Evening News)





Borussia Dortmund imeongeza maradufu mshahara wa kinda wa miaka 19 wa England Jadon Sancho hadi £80,000 kwa wiki ili kuzuia klabu nyengine kumwania. (Bild – in German)


Klabu za ligi ya Premia Manchester City, Tottenham na Arsenal zinamchunguza kinda wa Renne mwenye umri wa miaka 16 Eduardo Camavinga ambaye aliiongoza klabu hiyo kuilaza PSG 2-1 katika ligi ya daraja la kwanza Ufaransa siku ya Jumapili. (Mail) 


Monaco imekubali kumsaini kiungo wa kati wa Gabon na Southamptoon Mario Lemina 25 kwa mkoipo wa muda mrefu huku ikiwa na fursa ya kumnunua kabisa.. (RMC – in French)


Liverpool imekataa mwenendo wa klabu ya Denmark Nordsjaelland kumchukua mshambuliaji Bobby Duncan, 20, kwa mkopo wa muda mrefu. (Mail)


Besiktas imekubali makubaliano ya muda mrefu na klabu ya Tottenham kuhusu winga wa Ufaransa Georges Kevin N’koudou. (TRT Spor – in Turkish)


Klabu ya Ubelgiji ya Bruges inataka kumsaini kiungo wa kati wa Tottenham raia wa Kenya Victor Wanyama, 28. (Express)


Nahodha wa zamani wa klabu ya Manchester City Vincent Kompany amekosolewa kwa kujaribu kuiga mbinu za ukufunzi wa Pep Guardiola baada ya kushindwa mechi zake nne za kwanza kama mkufunzi mchezaji na klabu ya Anderlecht. (Mirror)





Juventus iko tayari kumjumuisha aliyeHSDPkuwa kiungo wa kati wa Liverpool Emre Can, 25,miongoni mwa mkataba kuwasaidia kumsaini mchezaji wa Barcelona na Croatia Ivan Rakitic 31. (Tuttosport, via Mail)


Mkufunzi wa zamani wa Ujerumani Berti Vogts amehoji uhamisho wa kiungo wa zamani wa Barcelona kuelekea Bayern Munich , akisema kwamba mchezaji huyo wa Brazil huenda hana uwezo wa kuwa nyota kama alivyokuwa siku za nyuma. (Goal)


Nahodha wa Ufaransa Hugo Lloris ameitaka Tottenham kuonyesha ukakamavu wa hali ya juu msimu huu huku ikitarji kushinda kombe la kwanza tangu 2008. (Standard)



Klabu ya Birmingham City imehusishwa na uhamisho wa beki wa kushoto wa Uhispania mwenye umri wa miaka 22 Alberto Redondo, ambaye aliachiliwa na Getafe mwisho wa msimu uliopita. (Footmercato, via Birmingham Mail)


Everton inapanga kucheza bila mashabiki mechi ya kirafiki ili kuwasaidia baadhi ya wachezaji wake wapya kuimarisha mchezo wao.. (Liverpool Echo)