Nchi 60 kushiriki maonyesho ya utalii tanzania.

Na Eric Msuya – MAELEZO
Zikiwa zimebaki siku 57 kufikia Tamasha kubwa la utalii hapa Nchini linalo fahamika kama “Swahili International Tourism Expo” ,Bodi ya utalii Tanzania TTB imethibitisha kuwa imejipanga vema kuwapokea wageni toka nchi 60 watakaoshiriki Tamashahilo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo , Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii, Devotha Mdachi ameeleza kuwa Tamasha hilo litafanyika oktoba 18 hadi 20 mwakahuu, katika Kumbi za Mikutano Mlimani City, huku mawakala zaidi ya 200 wakitarajiwa kushiriki katika Maonyesho hayo.
Hata hivyo, Devotha amesema juhudi za kufanikisha ujio wa wageni hao zaidi ya 200 kutokaNchi 60 zimefanywa kwa ushirikiano mkubwa kutoka Bodi ya Utalii TTB pamoja na Balozi zetu mbalimbali za nje.
“mpaka sasa tumepokea uthibitisho kutoka ofisi za ubalozi; toka nchi mbalimbali zikiwemo Ubalozi wa Sweden, Ubalozi wa Tanzania Nchini Malaysia, Ubalozi wa Tanzania Nchini China, Ubalozi wa Korea yaKusini, Ubalozi wa Japani, Ubalozi wa Kanada, Ubalozi wa Afrika Kusini, Ubalozi wa Omani, Ubalozi wa India, Ubalozi wa Uingereza, Ubalozi wa Brazili” Amezitaja Mkurugenzi Devotha.
Akieleza zaidi juu ya upokeaji wa wageni hao watakaofika katika Tamasha hilo, amesema wamejipanga na kujiboresha zaidi kwa kuwapeleka katika maeneo mbalimbali ya utalii nchini, ikiwemo Hifadhi ya Wanyama Serengeti, Uduzungwa, Mikumi, FukwezaTanga, Mapango ya Amboni, Mlima Kilimanjaro, Miradi ya Utalii wa Utamaduni mikoa ya Arusha na Kilimanjaro,piavisiwavya Zanzibar na Mafia.
Sambamba na hilo, kampuni na Mashirika mbalimbali zaidi ya 30 yamejitolea kuunga mkono juhudi hizo zinazo fanywa na TTB katika kuelekea kilele cha Maonesho hayo.
“kampuni kuu ambazo tayari zimetoa udhamini ni The Global Vector Control Standard, Benki ya CRDB ambayo ni mdau mkubwa katika sekta ya Utalii pamoja na shirika la Ndege la Ethiopia”
Mkurugenzi alitaja wadhamini wetu wakiwemo ni Air Tanzania, Hifadhi ya Taifa TANAPA, Mamlaka ya Hifadhi ya NgoroNgoro, Mamlaka ya Wanyama Pori Tower, Wakala wa Misitu TFS, na vyama vya Utalii.