Rais samia azindua na kukagua miradi ya kimkakati kwa utalii

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 15 Septemba, 2023 amezindua na kukagua miradi ya kimkakati iliyoko katika mkoa wa Mtwara ikiwemo Hospitali ya kanda ya kusini iliopo eneo la Mikindani, pembezoni mwa Bahari ya Hindi ambayo itahudumia mikoa ya Lindi na Ruvuma.

 Pia, amekagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mtwara  ambao ukikamilika utaweza kuhudumia ndege kubwa kama Boeng 220-300 suala ambalo litachagiza Utalii wa kusini hususani kurahisisha usafiri kwa  watalii kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo kanda ya  kusini mwa Tanzania.

Akizungumza kwenye ziara hiyo, Mhe. Rais Samia  amewataka watumishi wa Hospitali Rufaa ya Kanda ya Kusini pamoja na Uwanja wa Ndege Mtwara kufanya kazi  kwa weledi na tija ili kuleta ufanisi kwenye huduma wanazozitoa kwa wananchi na wageni.

Ziara hiyo ya Kimkakati imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ikiwemo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dustan Kitandula (Mb) ambaye anashiriki ziara hiyo itakayofanyika kwa siku sita katika mkoa wa Mtwara na Lind