Vodacom yazindua mashindano mapya kwa watengenezaji wa programu wa kujitegemea.

·         Mashindano yatatoa fursa kwa watengenezaji hao kuonyesha vipaji vyao.·         Mashindano kuwa katika awamu mbili,  ndani na nje ya nchi.·         Mshindi kupata dola 20,000. zaidi ya shilingi Milioni 30 za kitanzania.

Dar
es Salaam, Waendelezaji wa programu za kiteknolojia wa Tanzania sasa
watapata fursa ya kuonesha vipaji vyao katika mashindano yaliyo anzishwa
na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom, yaliyopewa jina la AppStar
Challenge.
 Mashindano hayo yameanzishwa ili
kuwapa motisha washiriki ambao wanaendeleza ubunifu wa kiteknolojia
katika simu na mawasiliano na kutoa nafasi kwa washiriki kuonyesha uwezo
katika kuvumbua vifaa mbalimbali vya kiteknolojia ambavyo vinaweza
kutumika katika nchi zinazoendelea na kutatua matatizo mbalimbali
yanayoikumba jamii.
Washindi watakao patikana katika
mashindano ya awali ndani ya nchi husika, watapata fursa ya kushiriki
katika mashindano ya kimataifa yatakayofanyika Afrika ya Kusini mwezi
Novemba mwaka huu. Nchi zitakazoshiriki katika mashindano hayo ni pamoja
na, Misri, Lesotho, Tanzania, Afrika ya Kusini na Qatar.
Katika
mashindano ya ndani, washiriki wanatakiwa kuendeleza ubunifu katika
vipengele mbalimbali kama michezo, afya ya jamii, burudani, na simu. 
Mshindi mmoja katika kila kipengele atapata dola 2000 za Marekani, na
baada ya hapo kwa mshiriki ambaye atakuwa ametoa programu bora atapata
nafasi ya kushiriki katika michuano ya kimataifa.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Kampuni ya
Vodacom Tanzania Kelvin Twissa, maombi yatawekwa na kusambazwa kupitia 
Hifadhi ya programu ya Vodacom na Vodafone  na watu binafsi kuendelea
kukusanya hadi mwisho wa muda wa kuwakilisha.
Twissa
alibainisha kuwa mshindi wa awamu ya kwanza ambayo inalenga Watanzania
tu, atadhaminiwa na Vodacom kushiriki katika mashindano ya kimataifa
yatakayo fanyika Afrika ya Kusini.
 “Awamu ya kwanza ni ya
mashindano ya ndani na watengenezaji wa programu wanatarajiwa kuanza
kujisajili kwa ajili ya mashindano kuanzia tarehe 7 mwezi 9 mwaka 2012
na wataweza kuziendeleza na kuzichapisha programu zao kwenye hifadi ya
programu ya Vodacom,” alifafanua Twissa.
Alibainisha kuwa
wakati wa michuano ya kimataifa, programu mbili zitakazoshinda
zitapelekwa katika mchujo utakaofanywa na jopo la wataalam wa kimataifa
wa masuala ya teknolojia kutoka Vodacom, zaidi ya hayo, wabunifu
watapata nafasi ya kuonyesha kazi zao kwa njia ya vitendo mbele ya jopo
la majaji.
 “Mashindano haya yatamuwezesha mshidi kupata
zaidi ya Dola elfu 20000 za Kimarekani. Tunajivunia kuwa sehemu ya
mashindano haya makubwa. Ninaamini kuwa yatatoa nafasi kwa watengenezaji
wa programu kuonyesha kile walichonacho, na ninatoa wito kushiriki
katika mashindano haya na tunawatakia kila la kheri,”