Ajiua kwa kunywa sumu baada ya kumuua mkewe na kumlaza kitandani
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao
 
Na Kadama Malunde – Malunde1 blog 
 
Mwanaume aitwaye Paschal Clement Mahona (32) mkazi wa Iponya kata ya Kagongwa wilaya ya Kahama amejiua kwa kunywa sumu baada ya kumuua mkewe Ashura Paschal (30) kwa kumnyonga shingo kisha kumlaza kitandani.Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao tukio hilo limetokea Agosti 28,2019 majira ya saa moja usiku.


“Ashura Paschal ambaye ni mkazi wa Iponya alikutwa akiwa ameuawa kwa kunyongwa shingo na kulazwa kitandani na mmewe aitwaye Paschal Clement Mahona mbaye naye baada ya kufanya mauaji hayo alijiua kwa kunywa sumu ambayo aina yake bado kujulikana na kukutwa chumbani akiwa amelala sakafuni, akitoa povu mdomoni”,amesema Kamanda Abwao.


“Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi kwani kabla ya tukio hilo wanandoa hao walikuwa wakigombana huku mume akimtuhumu mkewe kukosa uaminifu katika ndoa yao”,ameongeza Kamanda Abwao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *