Aweso aagiza wabadhirifu mradi wa maji kuwekwa mahabusu

Na Lucas Myovela, Arusha.

NAIBU Waziri wa Maji, Juma
Aweso (mb),ameamuru jeshi la Polisi wilaya ya Arumeru kuwakamata watumishi
watatu , wasimamizi wa mradi wa maji wa Makilenga uliopo katika tarafa ya
King’ori wilayani Arumeru Mkoani Arusha kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za
mradi huo.


Awali akielekea katika
chanzo cha mradi huo Aweso alisimamishwa 
njiani na wananchi wa kijiji cha Oldenyong’ilo kilichopo kata ya
King’ori Halmashauri ya meru ili waweze kueleza kero zao za maji hasa katika
mradi huo mkubwa wa maji uliojengwa kuhudumia tarafa hiyo yenye vijiji 22
katika kata tano.


Mmoja wa wananchi hao
aliyefahamika kwa jina la Mwaija Omary,alieleza kuwa kero ya maji katika kata
hiyo imekuwa sugu hasa kwa viongozi wasimamizi wa mradi huo  kuweka matabaka ya ugawaji maji kwa kupendelea
maeneo yao na kuwafungulia maji wananchi wengine pindi wanapo sikia kuna
viongozi wa serikali wanatembelea maeneo hayo.

“Sisi kama wananchi
tunaimani sana na mkuu wetu wa wilaya Jerry Muro ila watumishi na wasimazi
wakuu wa huu mradi wanatunyanyasa kama sisi siyo binadamu jana usiku wamesika
waziri anakuja ndiyo wametufungulia maji na siyo megi tumepata dumu mbili mbili
tu na maji tayari yamefungwa tunaomba mtuondolee watu hawa maana
watachonganisha wananchi na serikali yao.” walisema wananchi hao.

Mara baada ya Aweso
kumaliza kutembelea vyanzo vya maji hasa mradi huo wa maji wa Makilenga uliyo
gharimu fedha za serikali shilingi Bilioni 3.6 uliyo kamilika mwaka 2015 na kukabidhiwa
kwa wajumbe wa bodi ya maji ya Makilenga ili kuhudumia wananchi.

Mradi huo wa Makilenga
toka kukamilika kwake umeimarisha upatikanaji wa maji katika vijiji 22 katika
kata tano ambazo ni Ngarenanyuki,Leguruki,Kingo’ori,Maruango na Malula.Katika
kutoa huduma hizo Mradi huo unakusanya shilingi Milioni tano kwa kila mwezi
toka kuanzishwa kwakwe Mwaka 2015.

KICHEFUCHEFU
CHA HOTUBA YA MAKILENGA KWA NAIBU WAZIRI WA MAJI.

Naibu
waziri
: Nimesikiliza kwa makini hotuba yenu ila haijakamilika
kama nilivyo taka maana haina mapato na matumizi ya kila mwezi wala kila mwaka
nani mwasibu wa mradi huu wa Makilenga na Mwenyekiti wake.

Naibu
Waziri:
Je mwasibu mnakusanya kiasi gani cha fedha kwa
mwezi?, na Mmnesha kaa vikao vingapi vya mpango kazi,na wewe unamuda gani
kwenye mradi huu kama mwasibu?

Mhasibu:
tunakusanya
kwa mwezi shilingi Milioni tano Mh Naibu waziri na mpaka sasa hatujawahi kukaa
vikao na muda wangu katika mradi huu ni miaka mitano toka kuanzishwa kwake
nilikuwa mhasibu mpaka sasa.

Naibu
Waziri:
Je Mpaka sasa mnakiasi gani cha fedha toka 2015?

Mhasibu:
Miloni moja na Laki mbili Mh waziri.
Naibu
Waziri:
OCD chukua hawa watu weka ndani maana haiwezekani
toka mwaka 2015 hadi leo hakuna vikao wala mapato na matumizi na ukusanyaji wa
milioni 5 kwa mwezi hadi leo wanayo milioni moja na laki mbili pekee? Huu sio
mradi wa matumbo ya watu bali ni mradi wa wananchi na hakuna hata shilingi moja
itapotea.

Naibu
waziri:
Nimuombe fudi wa zamani Mzee Lemali aje hapa mbele.

Naibu
waziri
: Mzee wangu embu tueleze wewe ulivyo ondoka ulicha
account inashilingi ngapi za mradi na umeondoka lini.

Mzee
Lemali:
Mimi mpaka sasa nina miaka 3 toka niondoke katika
mradi huu na tuliacha Milioni 32 katika akaunti ya Mradi na mitambo ya nishati
ya Sola kwaa ajili ya kuendeshea na kusukuma pampu za maji.

Naibu
Waziri:
Mnaona sasa licha ya mradi huu wa makilenga kukusanya
Shilingi Milioni tano kwa mwezi lakini mpaka sasa fedha iliyopo bank ni Milioni
Moja na laki mbili pekee,Je nini maana ya makusanyo na wapi yanakwenda?

Walio kamatwa katika
sakata hilo ni Mwenye kiti wa mradi Bw Godhope Charles,mwasibu wa Mradi Bi
Waliaranga Kisetu na fundi msaidizi wa mradi Bw Ndekilo Kaaya huku meneja wa
mradi Bw Olenest akiponea chupu chupu baada ya kucheka mbele ya mkutano na
kushindwa kujibu maswali na kupewa adhabu ya kukaa masaa 12 kukaa rumande
katika kituo cha Polisi usa_river.

Kwa upande wake mkuu wa
wilaya ya Arumeru Jerry Muro amewataka wananchi kutokubeba maneno ya vijiweni
hususani katika suala la maendeleo na badala yake wawe chanzo cha maendeleo kwa
kuisaidia serikali kutunza miundombinu mbali mbali kwa ajili ya maendeleo.

Aidha aliagiza kuwa
kupitia mradi huu wa Makilenga wenye viti wote wa jiji 22 ambapo mradi huo
unatoa huduma ni lazima wawe kwenye bodi ya maji ya Makilenga ili iwe rahisi
kwa viongozi hao kuwasilisha na kutatua kero za wananchi wao kuhusu maji na
kupanga mgao sawa na sahihi kwa wananchi wote waliyopitiwa na mradi huo.

“Nilijua tunatatizo
katika kusimamia pamoja na ukosaji wa mfumo bora wa usimamizi wa usukumaji wa
maji lakinmi nilipo itisha kikao nikaambiwa mtaalamu wa mwanzo aliyekuwa
anashughulikia maji haya alitishiwa kuchomewa nyumba yake na yeye kuuwawa na
ndipo alipo kimbilia mkoani Iringa,”anasema.

Pia anasema” Ila nimemrudisha
kwa fedha zangu mwenyewe Mzee Lemali kwa ajili yeye ni mtaalam nani mzoefu wa
mradi huu anajua maji yanapatikana vipi na katika hili naapa hakuna jiwe
litakalo salia juu ya jiwe muda wenu sasa umekwisha tupo kwaajili ya
kuhakikisha wananchi wanapata maisha bora.” Anasema Dc Murro.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *