Breaking news, rais ateua katibu mkuu kiongozi mpya, mkurugenzi usalama wa taifa

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan usiku huu amefanya uteuzi wa Katibu Mkuu Kiongozi na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa huku akiwapangia kazi nyingine watendaji waliokuwepo katika nafasi hizo.

 Katika taarifa iliyotolewa na kusambazwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu Zuhura Yunus, Rais Samia amemteua Mosses Kusiluka kubwa Katibu Mkuu Kiongozi na kumteua Balozi Hussein Othman Katanga kuwa Balozi wa Tanzania mjini NewYork nchini Marekani na  mwakilishi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa.
Katanga anachukua nafasi ya Balozi Dkt Kennedy Gaston ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Pia Rais Samia amemteua Said Hassan Nassor kuwa Mkurugenzi mpya wa Usalama wa Taifa huku aliyekuwa mkurugenzi wake Diwani Athumani akiteuliwa kuwa Katibu Mkuu Ikulu.