Na mwandishi wetu, Musoma
Katika hali isiyokuwa ya kawaida imeelezwa kuwa watu wasiofahamika wamefyeka mazao kwenye mashamba ya baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi wa Serikali za mitaaa katika wilaya ya Butiama Mkoani Mara.
Taarifa hiyo ambayo bado haijathibitishwa, imeeleza kuwa tukio hilo limefanywa na watu ambao majina yao hayajapitishwa kwenye nafasi za kuwania uongozi kwenye maeneo yao katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika baadae mwezi huu.
Watu hao walikuwa wakiwania nafasi mbalimbali za uongozi za ujumbe katika ngazi ya uenyekiti wa Serikali za mitaa na majina yao kutopitishwa na viongozi wa uchaguzi kwa kigezo cha kukosea kujaza fomu za nafasi za ujumbe na uenyekiti wa Serikali za mitaa.