Breaking news: walioenguliwa kwenye uchaguzi serikali za mitaa butiama wadaiwa kufyeka mazao ya wasimamizi wa uchaguzi kwa hasira

Na mwandishi wetu, Musoma

Katika hali isiyokuwa ya kawaida imeelezwa kuwa watu wasiofahamika wamefyeka mazao kwenye mashamba ya baadhi ya wasimamizi  wa uchaguzi wa Serikali za mitaaa katika wilaya ya Butiama Mkoani Mara.

Taarifa hiyo ambayo bado haijathibitishwa, imeeleza kuwa  tukio hilo limefanywa na watu ambao  majina yao hayajapitishwa kwenye nafasi za kuwania uongozi kwenye maeneo yao katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika baadae mwezi huu.

Watu hao walikuwa wakiwania nafasi mbalimbali za uongozi  za ujumbe katika ngazi ya uenyekiti wa Serikali za mitaa na majina yao kutopitishwa na viongozi wa uchaguzi kwa kigezo cha kukosea kujaza fomu za nafasi za ujumbe na uenyekiti wa Serikali za mitaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *