Bunge iraq lapiga kura kuwafukuza wanajeshi wa kigeni baada ya marekani kumuua jenerali wa iran


Bunge
la Iraq limepiga kura kupitisha azimio linaloitaka serikali kuviamrisha
vikosi vya kijeshi vya kigeni kuondoa nchini humo. 

Hatua hiyo imechukuliwa katika kikao cha dharura kilichoitishwa leo. 


Azimio
hilo hasa linalenga kumaliza makubaliano yaliyoafikiwa mika minne
iliyopita yaliyoiruhusu Marekani kutuma vikosi vyake vya kijeshi
kusaidia katika vita vya kupambana na kundi linalojiita Dola la Kiislam
IS. 

Kura hiyo imepigwa siku mbili baada ya Marekani kumuua jenerali wa kijeshi wa Iran Qassem Soleiman akiwa nchini Iraq. 

Azimio hilo limeungwa mkono na wabunge wa madhehebu ya Kishia wenye mafungamano na Iran, ambao ndiyo wenye viti vingi bungeni