Dit waivalia njuga sekta ya afya, wahitimisha mafunzo ya utengenezaji vifaa tiba

 Na Mwandishi Wetu.

 Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kupitia Idara ya Ushauri wa Kitaalamu (ICB) leo imehitimisha mafunzo ya  wiki moja kwa mainjinia na Wataalam wa afya tisa (9) kutoka vituo mbalimbali vya afya nchini.



Akifunga mafunzo hayo, Naibu Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof. Patrick Nsimama amewataka wataalam hao kutumia vyema ujuzi huo ili waweze kuendana na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia na utoaji huduma kwenye sekta ya afya kwa jamii.


“Mafunzo haya yawasaidie ninyi lakini pia yawe chachu ya kulisaidia taifa kulingana na unyeti wa sekta ya afya kwa jamii, lakini pia mkasaidie wengine ambao hawajapata mafunzo haya kwa sababu ninyi mmekuwa wabobezi na hivyo mna uwezo wa  kuwajengea wengine uwezo….. wote mkawa  bora zaidi,”anasema.


Akizungumza kwa niaba wa washiriki wengine Riyaz Mohamed aliushukuru uongozi wa DIT kwa kuendesha mafunzo hayo kwani yamewabadilisha na kuwajenga japokuwa  muda ulikuwa  mfupi.


Mafunzo hayo yametolewa kwa wataalam tisa (9) kutoka mikoa ya Mara, Dodoma, Kilimanjaro, Mbeya, Pwani na Dar es Salaam.


Programu hii ni muendelezo wa kuwajengea uwezo wataalam wa afya ili kuweza kuenda na mabadiliko ya teknolojia na uhitaji katika utengenezaji wa vifaa tiba nchini

DIT