Figisu za madiwani ccm manispaa ya iringa zamwondoa meya madarakani….


MKAKATI  wa madiwani wa     Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  wa  kumwondoa  mstahiki meya  wa Halmashauri hiyo Alex  Kimbe kupitia  chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)   umetimia  baada ya  kura 14 za  ndio  kati ya  kura zote haliali 26  zilizopigwa kutumika  kumwondoa meya huyo  katika nafasi yake .

Katika  kikao  hicho  maalumu  cha  baraza la madiwani  kilichoitishwa  kwa  ajili ya kumwondoa meya  Kimbe  leo  ambacho kilifanyika chini ya ulinzi mkali wa  polisi na utaratibu  wa wajumbe  wote  wa kikao hicho kuingia kwa  barua maalumu ya mwaliko tofauti na vikao  vilivyopita ,madiwani  wa CHADEMA   hawakuweza  kuandika chochote katika karatasi ya  kupigia  kura  pamoja na maelekezo ya zoezi hilo kuwataka wapiga  kura kupiga kura ya ndio ama hapana.Mwenyekiti wa kikao  hicho Joseph Ryata  ambae ni naibu meya wa Halmashauri hiyo  akitangaza matokeo ya  kura  zilizipogwa ambazo upande wa meya Kimbe katika  zoezi la wazi la  kuhesabu kura  hizo  aliwakilishwa na mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter  Msigwa na upande wa  madiwani wa CCM waliokuwa  wakimpinga meya  huyo  kuwakilishwa na diwani  Ibrahim Ngwada  ,alisema  kuwa  kura zote  26  zimepigwa na  kati ya kura  hizo kura 12 ziliharibika na  kura 14  ni  kura  za ndio  ambazo  zilimtaka meya    Kimbe  kuondolewa katika nafasi yake .

”  Ndugu  wajumbe   zoezi letu  la mchakato wa kupiga  kura za  kumwondoa meya Alex Kimbe  madarakani  limekwenda  vizuri baada ya  wajumbe  wote 26  kushiriki kupiga kura za  kutokuwa na imani na meya  na  matokeo kura  zilizoharibika ni 12 na  kura  za  hapana hakuna na kura  za  ndio ni 14   hivyo natangaza  rasmi  matokeo ya  kura  zilizopigwa  kura waliosema ndio  meya  aondoke madarakani  wajumbe 14  wameshinda hivyo n atangaza  rasmi  kuwa meya Alex  Kimbe  kuanzia  leo Machi 28 mwaka 2020  sio msitahiki meya  tena wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa hadi kufikia hapa kikao  kimefungwa ” alisema Ryata  huku  akifunga mkutano huo na kuondoka .

Akizungumza baada ya    kutangawa kuondolewa madarakani aliyekuwa mstahiki meya wa Halmashauri   hiyo Alex Kimbe  alisema  kuwa  kuwa kimsingi  yeye  bado ni meya wa Halmashauri hiyo  kwani  kikao hicho kimeshindwa  kuffikisha  wajumbe asilimia mbili ya tatu  ya wajumbe  wote   wote 26  waliopaswa kupiga  kura  ya ndio hivyo ataendelea  kuwa meya hadi hapo  taratibu nyingine  zitakapofanyika  za  kumuondoa na zitakazofikisha therufi  mbili ya kura  za ndio .

”  Wameshindwa  kunitoa katika nafasi yangu kwa sababu  wameshindwa  kufikisha mbili ya tayu ya  wajumbe  wote kama  ambavyo kanuni inasema  nilichokiona na kumsamehe  bure mwenyekiti wa  kikao  hicho naibu meya Ryata ulimi wake  umeteleza  badala ya  kutangaza mimi  bado nitaendelea  kuwa meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa yeye  ametangaza kuwa mimi  sio meya   kwani  kimsingi  therufi  mbili wajumbe wote katika Halmashauri hiyo ni 17  na hao walipaswa  kuthibitisha mchakato huo  kuendelea  na leo therufi mbili imezidi maana   tulikuwa madiwani  26   lakini  ili meya  ama mwenyekiti wa Halmashaurti aweze kuondoka madarakani kanuni  ipo wazi  kuwa wajumbe mbili ya  tatu ndio  wanapaswaw  kumwondoa meya  madarakani  na waliopiga  kura  za  kuniondoa wapo  14   kumbe ilipaswa  wawe  17 hivyo mimi bado meya “

Aidha  alisema kuwa katika  kikao hicho  wakati  ikisomwa taarifa ya matokeo ya  uchunguzi wa  tuhuma dhidi  yake   alinyimwa  haki ya  kujieleza  mbele ya  wajumbe  baada ya tuhuma  hizo  kutolewa jambo ambalo yeye  amelitafsiri  kama   limefanyika kwa maelekezo maalumu  kutoka  kwa viongozi wa juu wa serikali ya mkoa wa Iringa .

Kwani  alisema kuwa kanuni za Halmashauri hiyo  zipo wazi kuwa  mkutano wa kumwondoa madarakani  mwenyekiti  anayetuhumiwa  utaongozwa na makamu  mwenyekiti  isipo kuwa mtuhumiwa atapata nafasi ya  kujitetea mbele ya  wajumbe  baada ya tuhuma  dhidi yake  kutolewa  ila imekuwa  kinyume  baada ya  tuhuma  kusomwa hakupewa nafasi ya  kujitetea  zaidi ya kuelekea zoezi la kupiga kura .

Huku  kwa  upande  wake  mbunge wa  Iringa  mjini Mchungaji Peter  Msigwa alisema kuwa mbinu  ambayo  waliitumia  jana  kupiga kura ni mbinu kabambe ya  kubaini  wasaliti  ndani ya CHADEMA   baada ya  kupata  taarifa za ndani kutoka CCM kuwa  kuna mbinu ya  kuwanunua madiwani watatu ama zaidi  ili wapige kura  za ndio  za  kumwondoa meya madarakani na ndipo  walipoamua  kuja na mpango wa  wajumbe  12 wa CHADEMA kupokea karatasi ya  kupigia kura ya  kuiweka kwenye sanduku la kura  bila  kuandika chochote na zoezi hilo  kufanyika pasipo  kificho  kwa kila anayepewa  karatasi kulinyanyua juu  bila  kuandika na kisha kutumbukiza kwenye sanduku .

”  Tulitaka  kura  zetu  12  kuwa salama bila  kununuliwa lakini wakati  huo  huo sio kwamba hizo kura kura 12  hazijapigwa  zimepigwa  hivyo kura zilizopigwa ndani ya ukumbi ni kura 26  na zilizomtaka  meya aondoke ni kura zao CCM 14  na 12  ni kura   zilizoharibika na kanuni ipo wazi inamtaka meya  kuondoka kwa therufi  mbili ya  kura zilizopigwa si vinginevyo  walihitaji kura  nyingine tatu ambazo hawajazipata katika mchakato  wao  huo wa kumuondoa meya hivyo kitendo cha kumtoa meya kuwa  wamemtoa meya  ni kichekesho  maana  wamekosa  kura tatu ” alisema Mchungaji Msigwa .

Mbunge  Msigwa  alisema kuwa  wao wanatambua kuwa zoezi la kumtoa meya  limekwama  baada ya  kura 3 kukosekana na  hivyo meya bado  halali katika nafasi yake na ataendelea  kufanya kazi yake  kama kawaida  na wao kama CHADEMA hawatafanya  fujo  yoyote na  wanataka madiwani wa CCM kufuata  taratibu ili  kulinda demokrasia  nchini .

Alisema anashangazwa na  nguvu kubwa inayotumiwa na serikali ya CCM ya kumtoa meya  Kimbe  wakati kimsingi muda  uliobaki ni mdogo sana na ni vikao viwili  pekee  ndivyo vimesalia  ili  kuvunjwa kwa baraza la madiwani kabla ya kuingia katika zoezi la uchaguzi mwingine .

Kwa  upande wake   diwani wa CCM Nguvu  Chengula  na  Ibrahim Ngwada alisema kuwa  Chadema walikuwa  wametengeneza mbinu ya kutopiga  kura  ila  mbinu hiyo imekwama baada ya zoezi hilo  kufanyika kwa mafanikio kwa CCM maana  kura  zimeweza kuamua kumuondoa meya   huyo madarakani .

Alisema  kuwa  kitendo cha madiwani  kutopiga  kabisa  kura  kimetoa nafasi ya meya  kuondolewa madarakani  kwani walipaswa  kupiga  kura za  hapana na sio  kutopiga kura  kabisa na  hivyo  kuwataka  madiwani hao 12  watambue  kuwa wameungana na CCM kumwondoa meya  wao .

Ngwada  alisema kuwa  kukataliwa kwa meya huyo ni dalili mbaya kwa mbunge  Msigwa kuondoka katika uchaguzi  mkuu  ujao kwani kitendo cha Meya  kuondolewa na ishara ya mbunge  kutotakiwa katika jimbo la Iringa mjini na kuwa  tuhuma  zilizotolewa ambao ameshindwa  kuzijibu  zinaonesha wazi ni jinsi gani  ambavyo  meya   huyo  alitumia vibaya nafasi yake  kwa  kujinufaisha  mwenyewe na madiwani  wenzake wa Chadema na hivyo kuitaka  taasisi ya  kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kumchunguza meya Kimbe kwa ubadhilifu wa fedha  za Halmashauri  ambao  umebainika katika ripoti ya kiuchunguzi dhidi yake .

Mwanasheria  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  Nicholaus Mwwakasungura  alisema  kuwa kitendo ambacho  wamekifanyha  chadema cha kutopiga  kura ya hapana ama ya ndio ndiko kumetengeneza mazingira ya  kuonesha kura za hapana  zimeshinda katika mchakato  huo wa kumuondoa meya madarakani .

Hivyo alisema kuwa  azmio  la madiwani  lililotolewa kwa njia ya  kura  kwenye kikao  hicho maalumu  ni sahihi   hivyo uamuzi wa kura 14  za  ndio zilizomtaka aondoke madarakani ndio  unaopaswa  kuheshimika na kutekelezwa  kwa mujibu wa kanuni  za baraza la madiwani   la Halmashauri  hiyo .

”  Kutokana na kura  zilizotangazwa na naibu  meya  ambae  alikuwa akiongoza kikao   hicho Joseph  Ryata kwa kutangaza matokeo ya  kura 14  zilizoshinda na kura 12  zilizo haribika   hivyo  kura  za ndio za madiwani wa CCM zimeshinda  katika zoezi la kumng’oa meya Alex Kimbe madarakani  na kwa matokeo hayo ni wazi  kuanzia leo Machi 28 Meya  Kimbe ameondolewa madarakani na sio meya tena wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa na anapaswa  kukabidhi  ofisi ” alisema mwanasheria  huyo wa Manispaa ya Iringa Mwakasungura .

Awali  kabla ya kufanyika kwa  zoezi la  kupiga kura  za  kumwondoa meya  Kimbe mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Himid Njovu aliwasilisha ripoti  ya uchunguzi wa tuhuma dhidi ya meya  na kuwa  uchunguzi  uliofanywa ulibaini  kuwa tuhuma  zote  zilizotolewa tuhuma  zaidi ya tatu  zina ukweli   na meya  alipoitwa kutakiwa  kujibu tuhuma  hizo  aligoma kutoa maelezo kwa madai jambo hilo halikufuata utaratibu .

Alisema  kuwa  timu ya uchunguzi  imebaini  kuwa mstahiki meya Alex Kimbe anamiliki  mali  nyingi ambazo zipo  katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Iringa na nje ya mkoa na baadhi ya mali hizo ni  shamba  kubwa  lenye  ukubwa wa ekari 30  lililopo  katika mataa wa CHautinde kata ya  Isakalilo ,Shamba kubwa  lenye  ekari 35  lililopo Pawaga  ambalo analitumia  katika kilimo cha Mpunga ,Shamba  kubwa  ekari 9 lililopo Pawaga ambalo pia analima mpunga , Shamba ekari 6 mtaa wa Kitasengwa kata  yake ya Isakalilo  na mashamba  mengine  yaliyopo  Kilolo  na nje ya  mkoa wa Iringa  pia  ana nyumba  tatu  ,gari aina ya Nadia  ambavyo  vyote  hivyo  alipata kati  ya mwaka 2015 na 202o kipindi  akiwa Meya 

”  Imebainika kuwa meya  Kimbe anamiliki mali  ambazo haziendani na  kipato chake  kwani kipato chake  kwa mwaka ni wastani wa  shilingi milioni 15  fedha  inayohusisha  na posho  za  vikao ,posho  ya madaraka,takrimu pamoja  na posho za vikao  na  shughuli za kilimo ,fuka la vipuri na  biashara  ya  wakala wa VODA ni vyanzo hafifu vya mapato  ya meya  huyo kuweza  kumiliki mali hizo .

Pia  alisema eneo  jingine ni la Chautinde  lenye  ukubwa wa zaidi ya ekari 25 maeneo hayo yapo  ndani ya kata anayoiongoza ya  Isakalilo   kuwa Manispaa  ya Iringa iliweka mpango wa uendeshaji wa  skimu ya umwagiliaji  kuelekea  eneo hilo ila meya  huyo  alinunua eneo  la Mtwivila (mkoga ) eneo  hilo lipo jirani na eneo linalomilikiwa na Fredrick Luvinga ambae ni rafiki wa  meya  kimsingi maeneo yote mawili yapo kwenye mpango wa uendelezaji wa skimu   kwa ajili ya wananchi  hivyo kujimilikisha ni kuwanyima fursa wananchi .

Aidha  alisema Kimbe analo eneo jingine ambalo lipo katika eneo  ambalo Halmashauri  inakusudia kulitoa kwa  ajili ya wizara ya afya ili  liweze  kujengwa Hospitali ya mafunzo kwa vitendo  kuwa  timu ya uchunguzi  ilijiridhisha kuwa  maeneo  yote mawili yanamiliki kihalali na meya  Kimbe  ameyapata  akiwa katika nafasi yake .


” Timu ya uchunguzi  imebaini  kuwa  Kimbe ana urafiki wa karibu na Frederick Luvinga  urafiki wao  ni wa muda hata kabla ya  kuwa meya  na  wawili hao  ni wakazi wa mtaa wa Kihondombi  A  kata ya Isakalilo  inayoongozwa na meya huyo  na timu ya uchunguzi  imejiridhisha  pasipo shaka  kuwa jengo la abiria katika  stendi ya Igumbilo nilalo jengwa na Luvinga wa kampuni ya yake ya ukandarasi ya Mwakalu Company  Ltd  na kimsingi  jengo lilipaswa  kujengwa  na Local Fund na siyo kampuni ”

 Kuwa  jengo hilo Luvinga na kampuni yake anatekeleza kazi nyingine  ya ujenzi  wwa sekondari ya kata ya Isakalilo  inayojengwa  katika eneo la Kitasengwa  kazi  hiyo  anaitekeleza kwa utaratibu wa Force Account kwwa gharama  ya shilingi 33,210,000 ambapo  anajenga  madarasa  sita kwa shilingi 33,210,000  na vyoo vya matundu 16.

Kuwa  zabuni ya kazi hiyo  ilitangazwa  na baadae  kamati ya ujenzi ya kata ya Isakalilo  ilipitisha  maombi tarehe 4/11 mwaka 2019 kumteua Luvinga kufanya kazi hiyo  wakati  kwa mujibu wa  kifungu  cha 60 (4) cha sheria ya ununuzi katika sekta ya umma ,mkataba  wowote  kabla haujasainiwa  unatakiwa  kupata  kibali  cha kamati ya  fedha na uongozi ambayo mwenyekiti wake Mstahiki meya  pia hata jengo la abiria Igumbilo meya  aliidhinisha mkakaba kuwa Luvinga afanye kazi hiyo  .

Kuhusu  tuhuma  za  rushwa  ya ngono  zinazomkabili meya  huyo  alisema timu ya  uchunguzi imebaini kuwa meya  amekuwa akimlazimisha  mapenzi Nancy Nyalusi  kwa  kutumia madaraka  yake  ya umeya kinyume na kanuni namba 9(3) ya maadili  (mamlaka za miji ) ya mwaka 2000  na kuwa alifanya  hivyo ili kumsaidia kupata kazi ya ukusanyaji mapato   Katika halmashauri  hiyo .

katika maoni ya  matatu ya kamati  ya uchunguzi  ilipendekeza  mstahiki meya  Kimbe  kuwa anatakiwa wakati wote  anapotekeleza  majukumu yake  kuzingatia  sheria ,kanuni na taratibu   na kuwa na kiwwango cha  juu kabisa  cha  uadilifu  kama inavyosisitizwa kwenye kanuni ya 8(a) (b0 na kanuni  ya 9 ya kanuni ya maadili ya madiwani (mamlaka za miji ) za mwaka 2000.

Pia  kutokana na  kuthibitika  kuwa  tuhuma  nyingi zinazomkabili   mstahiki meya  huyo ,timu ya uchunguzi  inapendekeza  kuwa Halmashauri  iendelee  na mchakato  kama inavyoelekezwa kwenye kanuni  namba 5 (7) ya kanuni  za  kudumu  za Halmashauri  na maoni ya  mwisho  ni  kutaka  TAKUKURU  kuchunguza kwa kina mwenendo wa mstahiki meya Alex Kimbe hususani  mali  zake  na namna alivyozipata  ili  kubaini   na iwwapo  mali hizo  ni halali au  la hatua  stahiki  zichukuliwe  dhidi yake .


MWISHO