Hatimaye taso kanda ya kaskazini yapata uongozi .

Mjumbe wa Mkutano kutoka Same Mkoani Kilimanjaro akiuliza swali mgombea wa uongozi TASO
Wajumbe wa mkutano wa TASO kanda ya Kaskazini wakifatilia maelekezo ya upigaji kura toka kwa msimamizi wa uchaguzi
Mwenyekiti wa TASO Taifa Bwana Isdori Mwalongo akifafanua jambo

 

Na Mwandishi wetu,

Jumuiya ya Wakulima Tanzania “Tanzania Agricultural Society” (TASO), Kanda ya Kaskazini imepata uongozi wa kanda. Mnamo tarehe 17 ya mwezi wa 12 mwaka 2022, Mkutano Mkuu wa kanda ya kasakazini ulikaa katika uwanja wa nanenane, Themi, Njiro mkoani Arusha. 

Mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama wapatoa 44 wakiwakilisha mikoa mitatu Manyara, Arusha na Kilimanjaro inayounda, kanda ya Kaskazini.

Mkutano huo wa kanda ulikutana kwa ajenda moja tu ya kufanya uchaguzi, baada ya kuwa na viongozi waliokaimu nafasi za kanda kwa muda mrefu. Akifafanua Katibu wa TASO Taifa ndugu Herry Beji “kwa mujibu wa Katiba ya TASO ilielekeza kufanyika uchaguzi wa viongozi ngazi zote kila baada ya miaka mitano, kutokana na changamoto ya jumuia yetu hivyo kwa mujibu wa maazimio ya mkutano mkuu wa TASO Taifa imetulazimu kufanya uchaguzi sasa, ili tuwe na viongozi kamili na sio wale waliokuwa wakikaumu nafasi hizo” alisema. 

Uchaguzi huo ulisimamiwa na kushuhudiwa na viongozi wa kitaifa akiwemo ndugu Mwenyekiti Isdori Mwalongo, Makamu Mwenyekiti Joyce Mwanga. Mkutano mkuu wa kanda ya kaskazini, ulifanikiwa kuendesha uchaguzi wake nakujaza nafasi zilizo wazi za kanda, zikiwa ni nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu na Mtunza Hazina., zilizokuwa zikikaimiwa kwa muda mrefu.

Baada ya mchakato wa maandalizi ya uchaguzi kukamilika, wagombea wanne waliokidhi vigezo walinadi sera zao, kuulizwa mwaswali na hatimaye kuomba kura kwa wajumbe wa mkutano huo, nakupigiwa kura.

Msimamizi wa uchaguzi, ambaye ndiye katibu TASO Taifa ndugu Herry Beji baada ya kuhesabu kura alitangaza matokeo kama ifuatavyo, Daktari Isdori Tarimo kutoka Rombo mkoani Kilimanjaro alitangazwa kuwa ndiye Mwenyekiti wa TASO kanda ya Kaskazini kwa kupata kura 41 sawa na asilimia 93.2 ya kura zote zilizopigwa. Ndugu Patrice Gwasma, kutoka Babati, mkoa wa Manyara, ametangazwa kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kupata kura 44 sawa na asilimia 100 ya kura zote zilizopigwa. Bi Ansila Marandu kutoka Arusha, mkoa wa Arusha ametangazwa kuwa Katibu, kwa kupata kura 43 sawa na asilimia 97.7 ya kura zote zilizopigwa. Na ndugu Nhojo Kushoka, kutoka Arumeru, mkoa wa Arusha ametangazwa kuwa Mtunza Hazina kwa kupata kura 44 sawa na asilimia 100 ya kura zote zilizopigwa.

Akitoa nasaha kwa viongozi hao wa TASO kanda ya kaskazini Bi Joyce Mwanga Makamu Mwenyekiti TASO Taifa amewataka viongozi hao kuchapa kazi na kurudisha umoja na imani ya wanachama juu taasisi yao. “ni wajibu wenu sasa kufanya kazi kwa nguvu na weledi, kwa kuzingatia Katiba, kuleta umoja wa kurudisha imani ya wanachama juu ya taasisi yao, kwani umoja huleta ushindi na kusonga mbele kwa pamoja” alisema.

Nae ndugu Isidori Mwalongo Mwenyekiti wa TASO Taifa, alitilia mkazo kwa kusema ushirika wetu ndio ushindi wetu kisha akasema “ uhai wa TASO upo mikononi mwenu” akieleza kisa cha mtu mmoja aliyetaka kumuumbua profesa mmoja kwa kumpima kama ana akili au lah. Yule mtu alimshika ndege mkononi na kumuuliza profesa kwamba kama una akili kweli nijibu swali hili je huyu ndege niliemshika mkononi yu hai au yu mfu? profesa akamjibu yule mtu kwa kumwambia kwamba uhai wa ndegu huyo upo mkononi mwako. Hili lilikuwa jibu sahihi kwani kama profesa angelisema ndege amekufa basi yule mtu huenda akamuachia ndege akaruka zake na kuthibisha kwamba profesa hana akili. Hata kama profesa angelisema ndege yu hai, yule mtu bado alikuwa na uwezo wa kumminya ndege hadi kufa na kumuumbua profesa kwamba ndege hayupo hai.

Nao viongozi TASO kanda ya kaskazini waliochaguliwa na mkutano huo walitoashukrani zao za kuchaguliwa na kuaminiwa na wajumbe wa mkutano huo. Mtunza Hazina alisema shauku yake nikuibadilisha TASO kwa wanachama na jamii kwa ujumla.

 “Tunataka TASO iende zaidi ya maonyesho ya wakulima (nanenane) kwani hili ni lengo moja tu kati ya malengo mengi ya TASO, tunataka tuwe na miradi itakayowanufaisha wanachama wote wa ngazi zote” alisema Nhojo Kushoka.