Ifahamu historia ya mapuli kitina misalaba, mwandishi wa habari na mtangazaji

Mapuli Kitina Misalaba ni Mkurugenzi wa MISALABA
MEDIA lakini pia ni Mwandishi wa habari na Mtangazaji wa Radio Faraja FM ya
Mkoa wa Shinyanga.

Amezaliwa terehe 28.2.1999 katika kijiji cha Chamva
kata ya Idahina Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga, ni kijana mwenye hofu ya
Mungu ukifuatilia sana ni mtu ambaye anafanikiwa kwa kupitia changamoto nyingi.

 Ni kijana
ambaye anapenda sana kufanyakazi yaani mimi huwa namwita kilaka kwa sababu
majukumu anayoyafanya utagundua kabisa anauwezo na juhudi za kipekee ambapo ni
watu wachache sana wanaoweza kufanya mambo anayoyafanya.

 Ukifika Radio
Faraja FM anafanya kazi kila siku hana siku ya kupumzika kama tulivyo wazoea
watu wengine yaani kiufupi hana muda wa kupumzika hata kama hayupo kwenye
ratiba hawezi kukaa nyumbani.

Hata ukifuatilia historia yake tangu akiwa shule
alikuwa anasoma huku anafanya mambo mengi alikuwa mchezaji wa msanii wa Nyimbo
za Asili za Kisukuma huku nyumbani walimtegea kwenye kazi za nyumba baada ya
kufika sekondari aliokoka akaingia kwenye kwaya kwahiyo alikuwa anatoka shuleni
anaenda kwenye mazoezi ya kwaya kanisani lakini mwisho wa siku alifaulu.

Yupo kwenye kitengo cha habari Radio Faraja FM na anamchango
mkubwa sana kuanzia Jumatatu hadi Jumapili anatekeleza majukumu yake pamoja na
majukumu haya pia yupo kwenye ratiba ya kukesha vipindi vya usiku pamoja na
shifti mbalimbali za kusimamia vipindi hapo Radio Faraja.

Kwahiyo anafanya vitu vyote kwenye Online Media yake
inayoitwa Misalaba Media bila kuathiri majukumu yake kwenye Radio Faraja.

lakini haishii hapo tu anafanya kazi na Media
zingine ikiwemo Matukio Daima, Idawa Media pamoja na Arusha Press Club hebu
jiulize ni mtu wa namna gani huyu ndiyo maana mimi huwa namwita kilaka  kwa sababu hata kwenye habari anafanya kazi
na watu mbalimbali.

Mimi kila siku nasoma habari zake anazoweka kwenye
Misalaba Media uzuri wake anaweza kuandika habari za aina zote yaani za matukio
ya Ukatili, maafa, Siasa, uchumi, habari za kijamii ndiyo nyingi lakini pia
anaandika mpaka habari za sherehe mbalimbali yaani Mungu aendelee kumbariki
sana hata kwenye YouTube kila siku anaposti.

Mapuli Kitina Misalaba pamoja na kuendelea na kazi
yake ya uandishi wa habari na utangazaji pia anaendeleza kipaji chake cha mziki
ambapo anaimba nyimbo za bongo fleva akitumia jina la Map Master MKM.

Pengine huyu kijana amekosa mtu wa kumshika mkono
anaweza kufanya makubwa zaidi ya haya anayoendelea kuyafanya.

Mara nyingi naona namba yake ameiweka kwenye
mitandao yake ya kijamii hata wewe unaweza kuwasiliana naye ili uone
unamsaidiaje ili aweze kufikia malengo yake katika kuiokoa jamii ya kitanzania,
namba yake ni hii 0745594231