Iran yaiweka wizara ya ulinzi ya marekani kwenye orodha ya kundi la kigaidi….yaongeza bajeti kwenye jeshi lake la quds

Shirika la habari la Iran limesema, bunge la nchi hiyo leo limeitaja wizara ya ulinzi ya Marekani kuwa ni kundi la kigaidi.


Habari
zinasema, kwa mujibu wa kura zilizopigwa na wabunge wa Iran, idara zote
na kampuni zenye ushirika na wizara ya ulinzi ya Marekani, na makamanda
wa Marekani waliopanga na kumuua aliyekuwa kamanda wa kikosi cha Quds
cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC Bw. Qassem Soleimani,
wamewekwa kwenye orodha ya kundi la kigaidi. 

Kadhalika, Kiongozi Mkuu wa Iran  Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameidhinisha kukiongeza Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Yuro milioni 200.

 

Khamenei,
jana usiku aliidhinisha kutolewa fedha hizo kutoka kwenye Hazina ya
Maendeleo ya Taifa kwa ajili ya Kikosi cha Quds cha SEPAH.


Aidha katika kikao hicho cha leo, Wabunge wa Iran wamepitisha kwa kauli
moja hoja ya “Kulipa Kisasi ‘ ambayo itaandaa mazingira kwa Iran
kulipiza kisasi dhidi ya Marekani  kwa kumuua Jenerali Qasse Soleimani,
aliyekuwa Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *