Iran yawakamata walioidungua kimakosa ndege ya ukraine

Msemaji
wa idara ya sheria ya Iran Gholamhossein Esmaili amesema, Iran
imekamata baadhi ya watu kutokana na kuhusika kwao katika ajali ya ndege
ya Ukraine iliyosababisha vifo vya watu 176 waliokuwa ndani ya ndege
hiyo.


Akizungumza
na waandishi wa habari, Bw. Esmaili amesema mpaka sasa uchunguzi kuhusu
wahusika umefanyika, na wataalamu wa sheria wanajitahidi kuhoji,
kuchunguza na kukusanya taarifa.

Amesema sanduku jeusi limepelekwa Ufaransa, na wataalamu wa Iran na Ukraine watashiriki kwenye kazi ya kusoma data.

Jumamosi
wiki iliyopita, jeshi la Iran lilisema, limeangusha kwa makosa ndege ya
abiria ya Ukraine, na kosa hilo la kibinadamu linapaswa kulaumiwa.