SERENGETI, NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII ATOA NENO
Na Mwandishi Wetu
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti iliyofanyika wilayani Serengeti mkoani Mara ambapo ndipo mitungi hiyo imekabidhiwa kwa wamama wajawazito, Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja kutolewa kwa mitungi hiyo ni ishara ya kwamba sasa tunahama na kuanza kutumia nishati ya gesi kwa ajili ya kupikia.
Hivyo amesema wanaishukuru kampuni ya oryx kwa kuendelea kuhamasisha usimamizi wa mazingira kwa kuachana kabisa na ukataji miti na uchomaji wa mkaa huku akieleza kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii inayosimamia misitu inahamasisha wananchi wote kurudi kwenye nishati mbadala , badala ya kukata miti na kuharibu mazingira yanayosababisha mabadiliko ya tabianchi ni vema tukatumia nishati mbadala itakayosaidia kutunza mazingira ili mazingira yatutunze.
Kwa upande wake Meneja wa Oryx Peter Ndomba baada ya kukabidhi mitungi hiyo ametoa rai kwa viongozi wa ngazi mbalimbali nchini kujenga utamaduni wa kutoa zawadi ya mitungi ya gesi kwa akina mama ambao wamekuwa wakipata changangamoto kubwa ya kutafuta kuni kwa ajili ya kupikia, huku akieleza iwapo mila zitaruhusu mwanaume anapokwenda kuoa badala ya kutoa ng’ombe au mbuzi basi awe anatoa zawadi ya mitungi ya gesi.
Akizungumza kwa niaba ya wanawake wajawazito Wilaya ya Serengeti ambako tukio la kukabidhiwa kwa mitungi hiyo limefanyika wakati wa Siku ya Maadhimisho ya Mtoto Njiti yaliyoratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Mwakilishi huyo ameishukuru kampuni ya Oryx kwa kuwapatia mitungi ya gesi kwani wameona haja hiyo kutokana na kipindi hiki kigumu ambacho wanakipitia wamama hao.
Awali Doris Mollel ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation ameelezea sababu ya kuomba mitungi hiyo ya gesi kukabidhiwa kwa wanawake wajawazito kwani anatambua changamoto ambayo wanawake hao wanaipitia, hivyo ni vema wakaachana na kutumia muda mwingi kufikiria kutafuta kuni na badala yake wawe na nishati safi ya kupikia ambayo pia itamuhakikisha usalama wake na kiumbe kilichopo tumboni.