Kampuni ya oryx yakabidhi mitungi ya gesi kwa wajawazito

 

SERENGETI, NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII ATOA NENO

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja (watatu kulia) akipokea mtungi wa gesi kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Oryx Peter Ndomba(wan ne kushoto).Tukio hilo limefanyika jana eneo la Rubanda wilayani Serengeti mkoani Mara wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti iliyoratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation ambayo imejikita katika kusaidia mtoto njiti na lengo la mitungi hiyo ni kuwawezesha wanawake kutumia nishati safi ya kupikia.

KAMPUNI Oryx Energies imekabidhi mitungi ya gesi 200 kwa wanawake wajawazito Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kama hatua za kuhakikisha mama mjazimto anatumia muda mwingi kulea ujaziuzito sambambamba na kutunza mazingira kwa kutokata miti kwa ajili ya kupata kuni za kupikia.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti iliyofanyika wilayani Serengeti mkoani Mara ambapo ndipo mitungi hiyo imekabidhiwa kwa wamama wajawazito, Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja kutolewa kwa mitungi hiyo ni ishara ya kwamba sasa tunahama na kuanza kutumia nishati ya gesi kwa ajili ya kupikia.

Hivyo amesema wanaishukuru kampuni ya oryx kwa kuendelea kuhamasisha usimamizi wa mazingira kwa kuachana kabisa na ukataji miti na uchomaji wa mkaa huku akieleza kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii inayosimamia misitu inahamasisha wananchi wote kurudi kwenye nishati mbadala , badala ya kukata miti na kuharibu mazingira yanayosababisha mabadiliko ya tabianchi ni vema tukatumia nishati mbadala itakayosaidia kutunza mazingira ili mazingira yatutunze.

Kwa upande wake Meneja wa Oryx Peter Ndomba baada ya kukabidhi mitungi hiyo ametoa rai kwa viongozi wa ngazi mbalimbali nchini kujenga utamaduni wa kutoa zawadi ya mitungi ya gesi kwa akina mama ambao wamekuwa wakipata changangamoto kubwa ya kutafuta kuni kwa ajili ya kupikia, huku akieleza iwapo mila zitaruhusu mwanaume anapokwenda kuoa badala ya kutoa ng’ombe au mbuzi basi awe anatoa zawadi ya mitungi ya gesi.

Doris Mollel ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation akisoma jina la mmoja ya wadau walioshiriki kufanikisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani wakati wa maadhimisho ya siku hiyo yaliyofanyika wilayani Serengeti mkoani Mara.

Akizungumza kwa niaba ya wanawake wajawazito Wilaya ya Serengeti ambako tukio la kukabidhiwa kwa mitungi hiyo limefanyika wakati wa Siku ya Maadhimisho ya Mtoto Njiti yaliyoratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Mwakilishi huyo ameishukuru kampuni ya Oryx kwa kuwapatia mitungi ya gesi kwani wameona haja hiyo kutokana na kipindi hiki kigumu ambacho wanakipitia wamama hao.

Awali Doris Mollel ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation ameelezea sababu ya kuomba mitungi hiyo ya gesi kukabidhiwa kwa wanawake wajawazito kwani anatambua changamoto ambayo wanawake hao wanaipitia, hivyo ni vema wakaachana na kutumia muda mwingi kufikiria kutafuta kuni na badala yake wawe na nishati safi ya kupikia ambayo pia itamuhakikisha usalama wake na kiumbe kilichopo tumboni.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Oryx Peter Ndomba (wa tatu kulia) akikabidhi mtungi wa gesi kwa mmoja ya wanawake wajazito wa Kata ya Rubanda kwa niaba ya wanawake wengine wajawazito wa wilaya ya Serengeti.Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja akishuhudia utolewaji wa mitungi hiyo ya gesi kwa wanawake wajawazito wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara.
Meneja Masoko wa Kampuni Peter Ndomba(kulia) akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Dk.Godwin Mollel wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti.Cheti hicho kimeandaliwa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa wadau hao katka kusaidia taasisi hiyo.

Naibu Waziri wa Afya Dk.Godwin Mollel (kushoto) akizungumza umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia baada ya Kampuni ya ORYX Energies kukabidhi mitungi ya gesi na majiko yake kwa wanawake wajawazito wilayani Serengeti kupitia Taasisi ya Doris Mollel Foundation.