Maelfu wakusanyika kwa maombolezo ya kamanda wa jeshi la iran qasem soleimani

Maelfu
ya waombolezaji wamekusanyika leo Jumamosi mjini Baghdad  kushiriki
maandamano ya mazishi ya kamanda wa jeshi la Iran Qasem Soleimani,
aliyeuawa katika shambulio la angani lililotekelezwa na Marekani siku ya
Ijumaa.


Wengi
wa waombolezaji walivalia nguo nyeusi na kubeba bendera za Iraq pamoja
na bendera za wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran ambao ni watiifu kwa
jenerali Soleimani. 

Soleimani alikuwa kiungo muhimu katika oparesheni ya Iran Mashariki ya kati na taifa hilo limeapa “kulipiza kisasi” mauaji yake.

Waandamanaji
walianza kukusanyika mjini Baghdad mapema asubuhi ya Jumamosi
wakipeperusha bendera ya Iraq naya waasi wakiimba “kifo kwa Amerika”.

Waandamanaji
walizunguka barabara za mji huo wakibeba mababgu yaliyo na picha ya
Soleimani huku wengine wakiwa na mabangu yaliyo na picha ya kiongozi
mkuu wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei.


Ripoti
zinasema mwili ya raia huyo wa Iran aliyeuawa katika shambulio hilo
utasafirishwa nchini humo Jumamosi jioni, ambako siku tatu ya maombolezo
imetangazwa kwa heshima ya jenerali.

Mazishi yake yatafanyika siku ya Jumanne nyumbani kwake Kerman eneo la kati la Iran.