Mahakama iringa yatoa uamuzi dhidi ya meya kung’olewa….

Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe kulia akiwa na wakili wake Barnabans Nyalusi leo baada ya mahakama ya hakimu mkazi Iringa kuondoa shauri lililofunguliwa na meya huyo kupinga kuondolewa madarakani 
Wafuasi wa Chadema na Meya Kimbe walivyowasili mahakamani leo 
Meya Alex Kimbe kushoto akitoka mahakamani baada ya maamuzi ya mahakama 
Wakili wa Kimbe Wakili Nyalusi kushoto akitoka mahakamani hapo na mteja waje


MAHAKAMA ya hakimu mkazi  Iringa  imeondoka   shauri  dogo namba 5 la mwaka  2020 lililofikishwa katika mahakama hiyo na  mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa kupitia  chama  cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA ) Alex  Kimbe  ya kupinga mchakato wa  madiwani  wa chama cha mapinduzi (CCM) kutoka  kumung’oa katika nafasi yake .

Akisoma    hukumu  ya kesi hiyo leo  hakimu  mkazi wa mahakama Iringa Aden Kanje  alisema  kuwa maombi   yaliyofikishwa mahakamani hapo  na mlalamikaji  huyo Alex  Kimbe ambae   katika kesi yake hiyo alikuwa  akitetewa na wakili Barnabans Nyalusi  vifungu  ambavyo   vilitumika  kufikisha maombi hayo vilikuwa  vimekosewa .

Hakimu  huyo  alisema  kuwa  hoja  za upande wa wakili wa serikali  alidai kuwa  hoja  za  mleta maombi mahakamani hapo  hazikuwa zimezingatia vigevyo  vya  kisheria hivyo  aliomba mahakama   hiyo  kutupilia mbali maombi hayo ya Kimbe  kutokana na  kutokidhi  vigezo  vya  kisheria pia  aliomba kupewa  gharama  alizozitumia katika  kufanya utafiti juu ya shauri hilo kutoka kwa mleta maombi mahakamani hapo  

Wakati  upande wa  wakili wa mleta maombi mahakamani hapo Barnabans Nyalusi  aliomba mahakama hiyo  kutoa  zuio la  kumng’oa meya  huyo madarakakani  kwa madai kuna taratibu  ambazo zinapaswa  kufanyika kabla ya kumwondoa meya  huyo madarakani .

Pamoja na  hoja  nne  ambazo zilitolewa na wakili wa  serikali  katika kupinga  maombi hayo  kusikilizwa na hoja  zilizotolewa na wakili  mlalamikaji  juu ya kupinga  hoja  za  wakili wa  saerikali mahakama  hiyo  imelitazama suala   hilo  kisheria na kitaratibu za kimahakama  na kuona hoja  za  upande wa  wakili wa serikali zina mashiko na  kuwa  hiyo haina mamlaka ya kusikiliza  shauri  hilo la  kuzuia kumng’oa meya madarakani .

Kwani  imeona maombi yake  yalitokana na hisia za  mwombaji wa zuio hilo kuwa yawezekana yasingefanyika  hivyo  na  kimsingi mahakama   kifungu   kilichotumiwa na mleta shauri hilo mahakamani  kilikuwa na makosa ya  kisheria .

Alisema  kuwa  kifungu namba 2(3)  kilichotumiwa  ni kifungu kinachosimamia  masuala ya  sheria  na mahakama ( Judicature and Apllication of Laws ( JALA )  kuwa  pamoja na  kifungo  namba 95 na 68 (E) vya  sheria  ya mwenendo  wa mashauri ya  madai .

Kuwa mahakama  hiyo haipati  nguvu ya  kimaamuzi katika  shauri  hilo  hilo  hivyo kwa  msingi  huo  maombi hayo yamekosa nguvu za  kisheria  hivyo mahakama  imelazimika kuyaondoa mahakamani hapo  na rufaa ipo  wazi ndani ya  siku 45  kwa  upande  wowote ambao utakuwa haujaridhika na uamuzi huo wa mahakama  kuwa  Mahakama  inaliondoa shauri  hili  kwa  gharama   za  uendeshaji  wa  kesi kwa  upande  uliopoteza .

Akizungumza na  wanahabari  nje ya mahakama hiyo  baada ya  hukumu  hiyo  kutolewa wakili  Nyalusi  alisema kuwa anakubaliana na uamuzi wa mahakama   na  kuwa  ambacho atakifanya  ni  kwenda  kuziangalia  hoja  ambazo zimetolewa  na mahakama katika  hukumu  hiyo  ili kuona namna ya kurudi mahakamani  hapo  .

”  Hakimu  hajafuta kesi  kwa  kutumia vifungu  ila amesema  vifungu  ambavyo  sisi tumevitumia  kuombea maombi  yetu  si sahihi  yeye  ametoa  kifungu  ambacho  lazima tukakisome  na  kuona maana  zipo kesi ambazo zimesikilizwa na mahakama kuu na kutumiwa  kifungu  hicho hicho alichokitoa yeye tunaamini  tutakwenda  kusoma na  tutashauriana  vizuri  na hii sio mwisho ”  alisema wakili Nyalusi .

Hata  hivyo  alisema kuwa  wao  walikuwa wanazuia mchakato wa  kumuondoa meya madarakani  sio  kuzuia meya kuondolewa  kwa kuamini kuwa mchakato huo haukufuata  sheria maana  kanuni za   Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  zinaeleza  wazi  ili meya  aondolewe  kuna taratibu za kufuata ila  hazikufuatwa   na  kwa kuwa  kilichojadiliwa  mahakamani si maombi yao ya msingi  ila kilichojadiliwa na kutolewa maamuzi ni taratibu  sio  hoja zao .

Hata   hivyo hivyo  alisema   kuwa hawezi kusema  zaidi  juu ya maamuzi ya mahakama  ila  wanakwenda  kujipanga  zaidi maana  hoja  zao za  msingi  mahakama  hiyo haijaweza  kuzigusia kabisa   zaidi ya  kutolea  uamuzi taratibu wa  za  ufikishaji wa maombi hayo mahakamani hapo .

Kuhusu  kuendelea kwa mchakato wa vikao vya  kutaka kumwondoa meya  madarakani  alisema kuwa wao hawajui kwanini mchakato huo unaendelea  kwani kimsingi kesi inapokuwepo mahakamani  watu  wenye hekima  huwa  wanasimamisha shughuli  zote  ila wanashangaa kuona  mchakato  ukiendelea  kuitwishwa .

Shauri   hilo la mstahiki  meya  Kimbe  kwenda  mahakamani kupinga  mchakato huo  wa kumwondoa  lilifikishwa mahakamani hapo Machi 17 kabla ya jana Machi 27   kutolewa maamuzi na mahakama  hiyo  japo wakati  mahakama  meya  huyo akiwa mahakamani hapo  mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Himid Njovu ameitisha kikao  cha dharua  cha  baraza la madiwani kitakachofanyika  leo baada ya  kikao kama  hicho  kilichokuwa na ajenda  ya kumung’oa meya  kushindwa  kufanyika  juzi kwa kukosa  mahudhuria ya  wajumbe 17  ambayo ni therufi mbili ya  wajumbe 26  ambao  walipaswa  kufika katika kikao hicho na badala yake  kufika  wajumbe 15  pekee .

Kabla ya  kuanza kwa  kikao   cha juzi  ambacho  kiliahirishwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Njovu   alisema  kuwa ili  kikao  hicho kiweze kuendelea  kwa  mujibu wa  kanuni namba 9,2  kanuni ya  kudumu ya Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa za  2015  zinaeleza kwamba akidi ya  wajumbe wa mkutano maalum wa Manispaa  hiyo itakuwa ni  therufi mbili ya  wajumbe  wote  na itahesabiwa  wakati wa ufunguzi wa mkutano .
“ Kwa  kanuni  hiyo  naomba ndugu  mwenyekiti na CC (katibu wa kikao) wetu  atuhesabie wajumbe  waliopo katika mkutano  huu  na therufi mbili ya  wajumbe wa mkutano huo  na therufi mbili ya wajumbe 26   wa baraza la madiwani  la  Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa ni wajumbe 17  na kama  idadi hiyo itatimia basi mwenyekiti atafungua mkutano huo ili  uendelee na kama idadi haitatimia basi mwenyekiti na baraza lake atatoa maamuzi atakayoona yanafaa”  alisema Njovu  na kukaa chini .


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *