Makamu wa pili wa rais zanzibar balozi idd aanza ziara mkoani shinyanga , akemea makundi ndani ya ccm kuelekea kwenye uchaguzi

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye pia ni Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, ameanza ziara ya siku tano mkoani Shinyanga, kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambapo pamoja na mengine  amekemea kuwepo na makundi ndani ya chama hicho.

Ziara ya Makamu huyo wa pili Zanzibar imeanza leo Agosti 19 wilayani Kahama kwa kutembelea Jimbo la Msalala, na kukagua utekelezeaji wa ilani ya uchaguzi ya  CCM katika jimbo hilo, ambapo kesho atakuwa jimbo la Ushetu na Kahama Mji.
Akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Buganzo kata ya Ntobo halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, amekemea kuwepo na makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM hasa kuelekea kwenye kipindi cha uchaguzi na kutaka kusiwepo na makundi hayo.
Amesema kuwepo kwa makundi ndani ya CCM, kuelekea kwenye kipindi hiki cha uchaguzi ni hatari, ambapo kutawagawa na kuwafanya kushindwa kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi na kuwapa nafasi wapinzani.

“Napenda kuwaambia wana CCM kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu ujao ushindi ni lazima, hivyo naomba kusiwepo na makundi ya aina yoyote ndani ya chama, pamoja na kutoweka wagombea wasio na sifa, bali pitisheni watu wanaokubalika kwa wananchi na waleta maendeleo,” amesema Balozi Iddi.


“Pia makatibu wa CCM ambao mna tabia ya kupitisha wagombea wenu wasio na sifa kwa sababu ya kufahamiana,naomba tabia hiyo muiache, kwani katika Serikali hii ya awamu ya tano tunataka washinde wagombea ambao wana sifa, waaminifu na wenye kuwatumikia wananchi kuwaletea maendeleo,”ameongeza Balozi Iddi.

Aidha amesema ili ushindi huo uweze kupatikana ni lazima watu wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura, pamoja na kwenda kupiga kura siku ya uchaguzi, na kuchagua wagombea wa CCM, ambao ndiyo wenye kupigania maslahi ya wananchi.
Katika hatua nyingine amewataka watanzania kudumisha amani pamoja kuuenzi Muungano, ili nchi iweze kuwa amani, kwa sababu bila amani nchi haiwezi kukua kimaendeleo kamwe.
Naye mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekiel Maige, akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi CCM jimboni humo kuanzia (2016-19),amesema jumla ya shilingi Bilioni 41.4 zimetumika kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ambapo hadi kufikia (2020) asilimia 90 ya ahadi zitakuwa zimetekelezwa.
Amesema miradi iliyotekelezwa ni ujenzi wa vituo vya afya, zahanati, ununuzi wa vifaa tiba, miradi ya maji, umeme ,pamoja na miundombinu ya barabara, huku miradi mingine ikiendelea kutekelezwa.

Na Marco Maduhu – Malunde1 blog


TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Makamu  wa Pili wa Rais  Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Buganzo kata ya Ntobo halmashauri ya Msalala na kukemea kuwepo na makundi ndani ya CCM hasa kuelekea kwenye kipindi cha uchaguzi, na kuwataka wawe kitu kimoja ili ushindi uweze kupatikana kwa kushinda viti vyote. Picha zote na Marco Maduhu – Malunde1 blog

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Buganzo Kata ya Ntobo halmashauri ya Msalala, nakuwataka watanzania wadumishe Amani pamoja na kuuenzi Muungano.

Mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekiel Maige akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha mapinduzi CCM kwa kipindi kuanzia (2016-19) na kusema jumla ya Shilingi Bilioni 41.4 zimetumika kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekiel Maige, akimuomba Makamu huyo wa Pili wa Rais Zanzibar kutoa msukumo Serikalini ili kufanikisha ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami kutoka Kahama kwenda Geita.

Mbunge wa jimbo la Msalala Ezekiel Maige akikabidhi taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa Makamu wa   Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kumaliza kuisoma.

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad, akimuahidi mlezi wa chama hicho Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Balozi Seif Ali Iddi kuwa ataendelea kushirikiana na wabunge mkoani humo kuendelea kuitekeleza ilani ya uchaguzi kwa kwaletea maendeleo wananchi zikiwamo huma za kiafya.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akielezea namna serikali mkoani humo inavyoendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kushirikiana na wabunge.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, akimuahidi Makamu Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga, kuwa maelekezo yote atakayo yatoa atayasimamia ili chama kiendelee kuwa imara.

Wananchi wa kijiji cha Buganzo Kata ya Ntobo halmashauri ya Msalala wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Wananchi wa kijiji cha Buganzo Kata ya Ntobo halmashauri ya Msalala ,wakiwa na Madiwani kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Wananchi wa kijiji cha Buganzo Kata ya Ntobo halmashauri ya Msalala wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye kijiji cha Buganzo Kata ya Ntobo halmashauri ya Msalala.

Wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye kijiji cha Buganzo Kata ya Ntobo halmashauri ya Msalala.

Wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye kijiji cha Buganzo Kata ya Ntobo halmashauri ya Msalala.

Awali Makamu wa Rais wa Pili Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa jengo la CCM Tawi la Buganzo.

Makamu wa Rais wa Pili Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi kiasi cha Shilingi milioni moja Taslimu mwenyekiti wa CCM tawi la Buganzo Lukas Shitungulu kwa ajili ya ukalimishaji wa jengo la ofisi la Chama kwenye tawi hilo.

Wanachama watano wa Chadema kwenye kijiji hicho ya Buganzo- Ntobo wakirudi CCM.

Getruda Boniphace aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema kijiji cha Buganzo, ambaye amejiunga CCM, amesema sababu za kurudi CCM kuwa alikuwa amepotea na kuamua kuunga juhudi za Rais John Magufuli.

Burudani za ngoma zikitolewa kwenye mkutano wa hadhara wa Makumu huyo wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye kijiji cha Buganzo Kata ya Ntobo- Msalala.

Awali Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwasili kwenye uwanja wa ndege Buzwagi wilayani Kahama Tayari kwa ziara mkoani Shinyanga ya kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwenye majimbo yote mkoani humo.

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisalimiana na mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa mara baada ya kushuka kwenye ndege kuanza ziara mkoani Shinyanga.

Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akisalimia na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, mara baada ya kushuka kwenye ndege tayari kwa ziara yake mkoani humo.

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum ambaye alifika kwenye uwanja wa ndege Buzwagi wilayani Kahama kwa ajili ya kumpokea na kumkaribisha mkoani Shinyanga, wapili kushoto ni mbunge wa jimbo la msalala Ezekiel Maige.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog