Msd kujenga kituo cha mauzo na usambazaji dawa simiyu

Mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD)  Laurean Bwanakunu akitoa neno la utangulizi katika mkutano wa tathmini ya utendaji kazi wa  Bohari ya Dawa(MSD) unaofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu kwa siku tatu  na lengo likiwa  ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu, Agosti 19, 2019.
Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifungua mkutano wa tathmini ya utendaji kazi wa  Bohari ya Dawa(MSD) unaofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu kwa siku tatu  na lengo likiwa  ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu, Agosti 19, 2019.
Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifungua mkutano wa tathmini ya utendaji kazi wa  Bohari ya Dawa(MSD) unaofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu kwa siku tatu  na lengo likiwa  ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu, Agosti 19, 2019.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Bohari ya Dawa(MSD), Victoria Mwanri Elangwa akitoa taarifa katika mkutano wa tathimini ya utendaji kazi wa  Bohari ya Dawa(MSD) unaofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu kwa siku tatu  na lengo likiwa  ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu, Agosti 19, 2019.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, bw. Jumanne Sagini (wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa idara mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa nchini(MSD) mara baada ya kufungua mkutano wao wa siku tatu, Agosti 19, 2019 ambao unafanyika kwa siku tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wakurugenzi wa idara mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa nchini(MSD) wakiwa katika mkutano wao wa siku tatu,uliofunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, bw. Jumanne Sagini  Agosti 19, 2019 ambao unafanyika  Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wakurugenzi wa idara mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa nchini(MSD) wakiwa katika mkutano wao wa siku tatu,uliofunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  Agosti 19, 2019 ambao unafanyika  Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wakurugenzi wa idara mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa nchini(MSD) wakiwa katika mkutano wao wa siku tatu,uliofunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, bw. Jumanne Sagini  Agosti 19, 2019 ambao unafanyika  Mjini Bariadi Mkoani Simiyu..
……………………..
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya dawa (MSD)  Laurean Bwanakunu amesema Bohari ya dawa inatarajia kuanza ujenzi wa kituo cha mauzo na  usambazaji  dawa mkoani Simiyu ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa mkoa wa Simiyu na mikoa jirani.
Bwanakunu ameyasema hayo Agosti 19,2019 katika ufunguzi wa  mkutano wa tathmini ya utendaji  kazi wa menejimenti na mameneja wa kanda wa bohari ya dawa nchini.
lengo likiwa   ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu.
Bwanakunu amesema wameamua kufanyia mkutano wa tathimini mkoani Simiyu ili kuweza kujionea eneo la ujenzi wa kituo cha mauzo ya dawa ikiwa ni moja ya kuongeza wigo mpana wa utoaji huduma.
“Tutakuwa na mkutano wa siku tatu hapa Simiyu kwa ajili kufanya tathmini ya utendaji kazi ulivyokuwa kwa mwaka mzima, tutawafanyia tathmini wakurugenzi wote na wenyewe watamfanyia Mkurugenzi Mkuu; lakini pia tutatumia fursa hii kutembelea mahali tulipoamua kujenga bohari kwa kuwa tunatarajia kujenga bohari hapa Simiyu”alisema Bwanakunu.
Akifungua mkutano huu, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema  maboresho ya usambazaji wa dawa yaliyofanywa na Bohari ya Dawa (MSD) yameongeza upatikanaji wa dawa mkoani Simiyu ambapo kwa sasa upatikananji wa dawa ni zaidi ya asilimi 88.
Aidha, Sagini ametoa wito kwa Taasisi zote za Umma zinazohitaji maeneo kwa ajili ya kujenga Ofisi zao kufika mkoani Simiyu, ambapo amewahakikishia upatikanaji wa maeneo lengo likiwa ni kuendelea kusogeza huduma mbalimbali karibu na wananchi.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa  Bohari ya Dawa(MSD), Bibi. Victoria Elangwa amesema uwepo wa kituo cha kusambaza dawa Simiyu kutapunguza umbali kwa Mkoa wa Simiyu na mikoa ya Mara na Shinyanga  kupata huduma za Bohari ambazo kwa sasa zinapatikana Mwanza.
Ameongeza kuwa ujenzi wa Kituo hicho unatarajia kuanza mara moja kwa kuwa tayari wataalam wameshaanza kushughulikia masuala ya ukamilifu wa mazingira na baada kukamilisha kazi hiyo atatafutwa mkandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi.